Michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka imeandaliwa na kampuni ya 4Beli kwa lengo la kukuza vipaji vya wanariadha chipukizi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya 4Beli, Dominic Mosha alisema jana katika uzinduzi wa mashindano hayo kuwa lengo la kuandaa michuano hiyo ni kuhamasisha vijana kuupenda mchezo wa riadha.
Mosha alisema fomu kwa ajili ya washiriki zitaanza kutolewa Julai 4 na kuongeza kuwa kutakuwa na mbio za kilomita 10 na kilomita 5 kwa ajili ya chipukizi wenye miaka mitano hadi 14.
Naye Katibu wa Shirikisho la Riadha nchini (RT), Ombeni Zavalla alisema mashindano hayo yameruhisiwa kufanyika kwa sababu waandaaji wametimiza vigezo.
Zavalla aliwataka waandaaji hao kuhakikisha wanatoa zawadi watakazozitangaza kwa washindi wote baada ya kumalizika kwa mashindano.










