Chini ya utawala wake uliodumu kwa miezi sita Simba, Kerr hakuwa na kikosi cha kwanza, jambo lililochangia kufungashiwa mabegi yake.
Katika kitu kinachoonekana kuwa tofauti kabisa na Muingereza huyo, Mayanja amesema anahitaji mechi mbili tu za kuwatathmini nyota wake kabla ya kuunda kikosi cha kwanza anachoamini kitakuwa na uwezo wa kuipa ubingwa Simba.
Akizungumza na Lete RAHA jana, Mayanja alisema baada ya mechi yao waliyoshinda 1-0 dhidi ya Mtibwa, amewaona wachezaji wake wanavyocheza, hivyo anahitaji kuwaona tena dhidi ya JKT Ruvu leo na ile inayofuata African Sport.
“Azam na Yanga kila moja imetupita kwa pointi sita, hizo si nyingi kwenye ligi, bado kuna mechi nyingi ambazo hazijachezwa. Ligi bado haijafika nusu, hivyo sina wasiwasi na tukijiweka sawa tutaweza kutwaa ubingwa,” alisema Mayanja.
Aliendelea kusema; “Tuna kikosi kikubwa na kinachohitaji kila mchezaji kujitambua na kucheza kwa kupambana kama kila mechi ni fainali. Tunaweza kufanikiwa.”
Mayanja kocha wa zamani wa Kagera Sugar na Coastal Union, alisema amefurahishwa na timu hiyo kutokana na wachezaji wake kuonyesha ushirikiano uwanjani.
Simba inapigania ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara katika misimu minne sasa.
Mayanja aja na kikosi cha ubingwa
20Jan 2016
Lete Raha
Mayanja aja na kikosi cha ubingwa
BAADA ya kuitazama timu yake katika mechi tatu za Kombe la Mapinduzi, kocha wa Simba, Jackson Mayanja, anajiandaa kufanya jambo litakalofunika kazi iliyofanywa kwa miezi sita na Dylan Kerr.
kocha wa Simba, Jackson Mayanja










