Wajibu wa Wakurugenzi wa kampuni

08Apr 2016
Denis Maringo
Nipashe
Wajibu wa Wakurugenzi wa kampuni

Utangulizi
Suala la uwajibikaji na uwepo wa menejimenti zipaswazo kutimiza majukumu yake ipasavyo limekuwa gumzo la wengi hapa Tanzania.

baadhi ya viongozi wakiwajibika kufanya usafi.

Katika miaka ya hivi karibuni mabilioni ya shilingi za ki-Tanzania, yakiwa fedha za waliowekeza na pia walipa kodi, zimepotea, katika makampuni binafsi na pia mashirika ya umma yanayojiendesha kama makampuni, ama vinginevyo.

Kutoweka masikioni mwetu mwa mashiurika kama lile la Nyama *Tanganyika Packers), Usagishaji (NMC), Makmaouni ya Biashara ya Mikoa (RTCs), cyama vya Ushirikia vilivyokuwa na mitaji na nguvu kubwa kama SHIRECU, na kadhalika, ni miongoni tu mwa kufa kwa taasisi za umma kunakoweza kuleta simanzi kubwa kwa yeyote mwenye uchungu na nchji yake.
Tume zimewahi kuundwa kuchunguza nini kilichotanda nyuma ya hasara kubwa katika kampuni hizi ambapo maswali mengi yaliyozuka ni pamoja na umma kuhoji uwezo wa uongozi katika menejimenti za mashirika haya na pia vitendo vya kifisadi vilivyofanywa na wale walioaminiwa kwa kupewa menejimenti zinazotawala mashirika haya. Suala lililo wazi basi ni kujiuliza iwapo upo ama hakuna wajibu wa kisheria ambao upo kwa wahusika wenye wadhifa kama Wakurugenzi wa makampuni, ya umma na yaliyo binafsi wanao.

Menejimenti za makampuni
Kampuni, ikiwa kama taasisi yenye taswira ya utu wa kutengenezwa (artificial person), inaweza tu kutekeleza majukumu yake kupitia watu halisi ambao katika lugha iliyo fasaha ni binadamu waliokabidhiwa kuendesha masuala kuhusiana na kampuni hiyo.

Watu hawa hujulikana zaidi kama “Wakurugenzi”, japo nafasi yao pale mahusiano kati yao na kampuni yenyewe yanapoangaliwa kwa karibu, inaweza kumchanganya mtu.

Ndiyo maana basi, hata tafisri za mahakama zimekinzana katika kuweka picha halisi ya wajhiobu wa Mkurugenzi hasa ni kwa nani: Kampuni yenyewe, wanahisa wake, wafanyakazi wake, wale waikopeshao (creditors), na kadhalika.

Hata hivyo kupitia tafsiri mbalimbali za mahakama katika sheria, picha kamili kuhusiana na swali hili imeendelea kueleweka zaidi.

Kisheria Wakurugenzi wa kampuni ni Mameneja wanaosimamia masuala ya kampuni (Rejea hukumu ya Aberdeen Railway Co. v. Blaikie Bros iliyoripotiwa mwaka 1854). Tofauti na wengi wawezavyo kufikiri, Wakurugenzi wa kampuni si watumishi wa kampuni husika. Jambo hili lilifafanuliwa kwa kina katika kesi maarufu ya M’Lintock v. Campbell (1916) SC 966, katika ukurasa wa 980.

Kwa lugha ya sheria ya bunge, neno ‘Mkurugenzi’ linamaanisha Mkurugenzi ama mtu yeyote anayefanya majukumu ya Ukurugenzi hata kama anapewa ama anajulikana kwa jina jingine.

Basi ukiweka pamoja katika lugha rahisi kile tulichokirejea japo juu, tunaweza kusema tu kwamba neno ‘Mkurugenzi’ lina maana ya yule ambaye kutokana na maelekezo yake maafisa wa kampuni hufanya kile wakifanyacho ama kupaswa kukifanya.

Nini hasa nafasi ya Mkurugenzi kisheria?

Kama tulivyoona hapo juu, si rahisi kutaja kwa maneno mafupi na moja kwa moja kuhusiana na Mkurugenzi wa Kampuni na nafasi yake katika kampuni husika. Mahakama, hata hivyo, katika azma ya kuyalinda makampuni kama taasisi, zimetoa msisitizo kwamba Wakurugenzi wana jukumu lenye sura mbili zilizo sambamba, yaani zikiwepo pamoja katika wakati ule ule.

Ndiyo kusema basi, Wakurugenzi wa kampuni ni Wadhamini wa kampuni, na wakati huo huo ni Mawakala wa kampuni hiyo hiyo katika uwepo wake na katika shughuli zake za kila siku.

Wajibu wa Wakurugenzi wa Kampuni
Msingi wa kazi za Wakurugenzi wa kampuni umekijikita katika mambo makuu mawili. Mosi,Wakiwa wamechaguliwa kuwa katika nafasi hiyo, Wakurugenzi wanabeba jukumu la raslimali fedha na raslimali nyingine za kampuni.

Kwa hili, itokeapo hakuna udhibiti mahsusi kisheria, Wakurugenzi wanakuwa huru kufanya takribani jambo lolote kwa namna yoyote katika raslimali za kampuni na namna zinavyotumika.

Wakiwa wadhamini, wanakuwa wakikabiliwa na wajibu alionao Mdhamini kufanya mambo kwa misingi ya dhamana iliyopo.

Kwa upande mwingine, tunaweza kusema kuwa ki-ukweli Wakurugenzi kwa uhalisia wanakuwa wamepewa mamlaka yasiyo na ukomo kupitia Ibara zilizoko katika Katiba ya Kampuni (Articles of Association). Misingi ya uwakala inahusika katika nguvu za kimamlaka za Wakurugenzi.

Kanuni za uwakala zinahusika katika utekelezaji wanguvu za mamlaka ya Wakurugenzi ambapo, kama mawakala, wanapaswa kutekeleza kazi zao kama Wakurugenzi kwa umakini, uhodari na kujiridhisha katika athari za kila wakifanyacho au kifanywacho katika kamopuni hiyo inapokuwa chini ya himaya yao.

Kabla hatujayaangalia majukumu haya ya Wakurugenzi kwa mapana yake ni vema tu kukumbuka mipaka ya wajibu ambayo Wakurugenzi wanakuwa nayo wanapoiongoza kampuni.

Katika hili ni muhimu sana tukikumbuka tena na tena kwamba, kisheria, wajibu na majukumu waliyonayo Wakurugenzi ni kwa kampuni yenyewe na si kwa mwana hisa mmoja mmoja wa kampuni. Hii ni kwa mujibu wa msingi uliowekwa zaidi ya karne moja iliyopita katika hukumu ya Percival v. Wright [1902] 2 Ch. 421, msingi ambao chimbuko lake hasa linaanzia katika kesi ya zamani kidogo iitwayo Foss v. Harbottle (1843) Hare 461.

Na isisahaulike pia kuwa Wakurugenzi wa kampuni, mara nyingi kupitia Bodi, ndio wenye jukumu la kuendesha shughuli za siku kwa siku za kampuni na si mwanahisa ambaye hana mamlaka hayo zaidi ya kufuatilia tu kile kinachofanywa na kampouni nap engine kuhoji, kupitia vikao na nguvu za kura yake, mara nyingi kulingana na idadi na pia aina ya hisa anazomiliki.

Ndiyo maana basi, hata kunapotokea kuboronga kwa Wakurugenzi, ni kampuni yernyewe inaytweza kumfungulia mashtaka Mkurugenzi au mfanyakazi. Mwana hisa hana nguvu hiyo, kwa kawaida.

Tuanze kwa kukiweka katika lugha rahisi, kile tulichokizungumzia hapo juu. Chukulia mfano wa kampuni mbili tofauti: Moja ikiitwa Tunakula Bata Limited ambayo ina wanahisa 2-500 wanaojumuisha watu na makampuni binafsi. Na halafu tena kuna kampuni nyingine ambayo (yaweza kuwa benki, kampuni ya saruji, vileo na kadhalika) ambayo wanahisa wake ni Serikali na makampuni mawili matatu hivi binafsi.

Kila moja kati ya kampuni hizi kwa kawaida inakuwa na Wakurugenzi wanaosimamia uendeshaji wake wa kila siku kuhakikisha uendeshwaji na ustawi wa kampuni hiyo vinakwenda sawia na dira, malengo na pia matarajio ya uanzishwaji wake, na ambapo mara zote kipimo huwa ni kujiendesha kwa tija, ushindani na zaidi kurejesha thamani na pia ziada katika kile kilichowekezwa na wanahisa.

Na takribani kampuni zote duniani huendeshwa katika dhana hii, iwe ni kampuni katika msingi wa kibepari ama wa Kijamaa, iwe nchi tajiri au maskini na bila kujali kama au la kampuni hiyo inauza au haiuzi hisa zake katika soko la mitaji.

Turejee tena katika mantiki ya kisheria tunayoendelea nayo hapa na hasa tulijibu swali hili: Inakuwaje basi tunasema kwamba wajibu wa Mkurugenzi wa kampuni ni kuitumikia zaidi kampuni yenyewe na si wana-hisa mmoja mmoja?
Profesa Florens D.A.M Luoga wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni anaheshimika sana nchini katika masuala ya sheria za kodi, mikataba na makampuni, anaainisha katika moja ya machapisho yake kuwa mahakama zimeona mantiki katika jambo hili kwa kubainisha kuwa ni wana-hisa wenyewe ndio wenye jukumu la kuchagua Wakurugenzi wa kampuni ambazo hisa zao zimo na “ iwapo wanaamua basi kuwaweka watu wasio na uwezo kuendesha biashara hizo, basi sheria haiwazuii kufanya hivyo.”

(Rejea Florens D.A.M. Luoga ‘Duties of Company Directors in Tanzania: The Need for Legislative Reform’, 18 Eastern African Law Review 247 (Juni 1991), No.2, na hasa katika ukurasa wa 249; aya ya 2.). Zingatia: Makala ya Profesa Luoga iliandikwa miaka kumi hivi kabla ya kuwepo kwa Sheria Mpya ya Makampuni ya mwaka 2002.

Tofauti pekee katika utekelezaji wa utaratibu huu hapa juu ni pale ambapo Wanahisa wanawachagua Wakurugenzi kama mawakala wao wa moja kwa moja kwa namna isiyo na utata kisheria, katika utekelezwaji wa jambo fulani. Inaonyesha basi kama inakuwa hivyo, basi Wakurugenzi wanapaswa kuwajibika moja kwa moja kulingana na matakwa na kwa wanahisa wenyewe kama zilivyo sheria za Uwakala.

Katika kesi moja ya New Zealand iitwayo Coleman v. Myers [1977] 2 NZLR, Mahakama ya Rufaa ilehukumiwa kuwa katika kubainisha iwapo au la kunazuka kuwepo kwa Wajibu wa Mkurugenzi katika mahusiano yake na Mwanahisa, uamuzi wa kuwepo kwa jambo hilo utatokana na kuyaangalia mazingira husika na aina husika ya wajibu unaotajwa kuwepo hapo.

Mtazamo huu umefafana pia na uamuzi ilitolewa na Mahakama nyingine katika kesi ya Gething v. Kilner iliyoripotiwa mwaka 1972 katika jarida la Sheria ya Uingereza liitwayo All E.R na lile la kila juma, la Uingereza pia, liitwalo W.L.R.

Sheria ya zamani ya Makampuni ya Uingereza (Companies) Ordinance (Sura ya 212) haikuwa na vifungu vya jumla vinavyoelekeza kwa kufafanua wajibu wa Wakurugenzi wa Makampuni. Kama jambo hili lilificha au kuchochea matukio ya kifisadi, kuchangia makampuni na mashirika kuendeshwa bila tija na hata kufilisika, ni historia pekee italitolea hukumu.

Ni vizuri hata hivyo, kama ambavyo tumeilinganisha Katiba ya nchi yetu na nyinginezo nzuri, tukailinganisha sheria yetu ya makampuni na kwingineko katika vipindi tofauti.

Mathalani, Wakati sheria yetu ikiwa kimya kuhusiana na wajibu wa Wakurugenzi wa makampuni (na pengine kuchangia kuleta dhana potofu iliyojengeka muda mrefu hapa nchini ambapo Mkurugenzi wa kampuni hujiaminisha kuwa kampuni ndiyo yeye na yeye ndiyo kampuni, kitu ambacho si kweli.

Katika hili rejea tu kesi ya Salomon v. Salomon, hukumu ambayo kama hutumika sana kuifafanua dhana ya kampuni katika lugha inayoeleweka zaidi kama ambavyo Injili ya Luka itumikavyo sana na Wakristo kote duniani pale suala la kifo na ufufuko wa Yesu Kristo linapoanza kusimuliwa.

Nchini Australia, sheria ya Makampuni ya nchi hiyo iliweka bayana wajbu wa Mkurugenzi/Wakurugenzi wa kampuni katika lugha hii (tunanukuu):

“Mkurugenzi, katika muda na nyakati zote anatumikia kwa uaminifu na atatumia umakini unaostahili katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake.”

(tafsiri ya haraka na isiyo rasmi kutoka kifungu kidogo 124 (1) cha Sheria ya Makampuni ya Australia, 1963). Kifungu hiki katika lugha yake halisia kimombo kiko hivi:

“A director shall at all times act honestly and use reasonable diligence in the discharge of the duties of his office.”
*Denis Maringo ni Mwanasheria aliyeko Dar es Salaam.

Simu: 0719270067; Barua-pepe: dnmaringo@gmail.com