'Wafungaji wa5 bora wa muda wote EPL

20Mar 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
'Wafungaji wa5 bora wa muda wote EPL

HARRY Kane ndiye mshambuliaji pekee anayecheza nafasi kubwa katika wafungaji (vinyozi) watano bora wa Ligi Kuu England maarufu kama EPL wa wakati wote.

Muuaji huyo wa Tottenham Hotspur amekuwa akihatarisha safu ya ulinzi ya timu pinzani tangu msimu wake mzuri wa 2014-15.

Lakini licha ya kudumisha kiwango cha kustaajabisha na kushinda Kiatu cha Dhahabu kwa ufungaji bora, bado ana njia ya kwenda kumwangusha kiongozi wa sasa katika viwango vya ubora, Alan Shearer.

Makala haya inawaangalia wachezaji watano ambao ni wafugaji bora wa wakati wote kwenye Ligi Kuu England.

 

#5. Sergio Aguero (Mabao 184)

Sergio Aguero atakuwa gwiji katika Klabu ya Manchester City baada ya kufunga moja ya mabao ya kipekee katika historia ya soka ya England dhidi ya QPR na kutwaa taji la Ligi Kuu mwaka 2012.

Kabla ya kuelekea Barcelona, ambako ugonjwa wa moyo kwa bahati mbaya ulimlazimu kustaafu mapema, Aguero aliweza kufunga mabao 184 katika mechi 275 pekee za Ligi Kuu England.

Muargentina huyo alishinda mataji matano ya ligi wakati alipokuwa Etihad na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Man City.

Fowadi huyo anashikilia rekodi ya Ligi Kuu England kwa hat-trick nyingi zaidi, akiwa amefunga mara 12, na ndiye mchezaji pekee wa kigeni nje ya England kwenye orodha hii.

 

#4. Andy Cole (Mabao 187)

Andy Cole hakuwa mgeni kwa kuzifumania nyavu kwenye Ligi Kuu England na alikuwa mwiba mkali kwa timu alizokutana nazo.

Kwa kweli, mshambuliaji huyu wa zamani wa Manchester United na Newcastle United alikuwa mfungaji mzuri na mpiga penalti mzuri zaidi.

Cole alifunga mabao 187 katika mechi 414 za Ligi Kuu huku akishinda mataji matano katika misimu yake nane akiwa na 'Mashetani Wekundu' hao.

 

#3. Harry Kane (Mabao 203)

Kane amekuwa kitovu cha safu ya ushambuliaji ya Tottenham Hotspur kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na amefunga angalau mabao 15 katika kila misimu tisa iliyopita.

Lakini licha ya uchezaji wake kwenye eneo la hatari, hajaweza kubeba taji lolote akiwa na Spurs na anahusishwa na kuondoka.

Pia mfungaji bora wa pamoja wa nchi yake akiwa na mabao 53, namba 10 wa uhakika kwa timu ya taifa na klabu yake na anaweza kupanda kwenye orodha hii kwani bado anacheza na yupo kwenye kiwango bora kabisa.

 

#2. Wayne Rooney (Mabao 208)

Wayne Rooney alimpita gwiji Bobby Charlton kama mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United na England, ingawa Kane yuko mbali na kumpita kwa upande wa timu ya taifa, maarufu Simba Watatu.

Katika mechi 491, gwiji huyo wa Old Trafford alifunga mabao 208 na kutoa pasi za mabao 103 kwa Everton na Mashetani Wekundu.

Bingwa mara tano wa Ligi Kuu, Rooney alifurahia maisha mazuri lakini amepungukiwa kwa kiasi fulani na mfungaji bora kwenye orodha hii.

 

#1. Alan Shearer (Mabao 260)

Huwezi kutaja wafungaji mabao wa Ligi Kuu England bila kumtaja Shearer mkubwa.

Akiwa amefunga mabao 52 zaidi kwa jina linalofuata kwenye orodha, rekodi ya mshambuliaji huyo wa England itazidi kiwango.

Kufunga mara 260 katika michezo 441 kwa misimu 14 akiwa na Blackburn na Newcastle, ni kiwango cha ajabu kwa mchezaji huyo aliyekuwa akivaa jezi namba 9 na alishinda taji moja tu na tuzo nne za Mchezaji Bora wa Mwezi.

Shearer ndiye mchezaji mwenye kasi zaidi kugonga karne moja kwenye Ligi Kuu - akichukua michezo 124 pekee na anasalia kuwa mchezaji pekee kufunga zaidi ya mabao 30 katika mismu kadhaa kwenye Ligi Kuu.