Hayo yamebainishwa na Daktari wa mifugo na mtafiti mwandamizi wa wakala ya maabara ya mifugo tanzania kanda ya ziwa Ronald Benju kwenye maonyesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi inayofanyika katika Viwanja vya Nyamuhongolo mkoani Mwanza ambapo ameeleza ufugaji ni biashara ambayo inapaswa kutendeka kwa kufuata maelekezo muhimu kutoka kwa wataalamu.
Anaeleza wana vifaa vya kupima aina mbalimbali za sampuli zinazo wezesha kubaini aina za magonjwa yanayo kabili mifugo na kutoa matibabu sahihi ikiwa ni pamoja na kupima na kuthibitisha viwatilifu vya mifugo vikiwemo vya kuulia wadudu kama kupe ambavyo mara nyingi vimekuwa viki lalamikiwa na wananchi kuto kufanya kazi.
‘’Tunashukuru tumejaribu kutoa elimu kwa jamii na naona wafugaji wanaendelea kutuelewa ,sasa hivi tunawekeza nguvu kuelimisha wananchi wa maeneo ya mbali ‘’alisema
Vilevile maabara hiyo inapima ubora wa chakula cha mifugo ili kuwezesha mifugo kupata chakula kinacho bora kitakacho wezesha mifugo kuendelea kukua vyema na kutoa tija kwa mfugaji.
Afisa mifugo mwandamizi aliye katika shamba la mifugo Mabuki Lini Mwalla amewataka wafugaji kutumia mbegu bora za mifugo zinazo tolewa na serikali katika mashamba yake kama hatua ya kuongeza tija ya uzalishaji na kumsaidia mfugaji kunufaika kupitia rasilimali hiyo ambayo kwa sasa wengi wao wamekuwa wakifanya shughuli hiyo kwa tija ndogo.
‘’Tunatamani kila mfugaji anufaike na rasilimali hii serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kuwezesha wafugaji kuongeza tija hivyo wanapaswa kuitumia vyema fursa hiyo’’amesema Dk Mwalla.
.
Sunday Mtaki mkazi wa Mwanza ambaye ni mfugaji wa kuku ametembelea banda la wakala wa maabara ya veterinari Tanzania kanda ya ziwa kupata elimu juu ya masuala ya maabara ya mifugo ambapo ameeleza elimu zaidi inapaswa kutolewa ili jamii ifahamu uwepo wa huduma hiyo kwani wengi bado hawana uelewa.
‘’Nimepata elimu kuhusu chanjo mbalimbali za mifugo na unapaswa upeleke sampuli kwenye maabara ya mifugo kama mifugo ikipata magonjwa ili kujua matibabu sahihi na kutibu’’ Alisema Mtaki
Aidha ameomba elimu zaidi kutolewa kwa wafugaji ili wafahamu uwepo wa maabara hiyo pamoja na serikali kuongeza idadi ya maabara za mifugo hatua itakayo punguza adha ya wananchi wanaoishi nje ya mkoa wa Mwanza kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo mkoani Mwanza.
Mfugaji mwingine wa ng’ombe Pius William mkazi wa mkoani Mwanza anaeleza kabla ya kupewa elimu ya namna ya ufugaji bora alikuwa na wasiwasi wa namna ya kufuga katika eneo dogo lakini baada ya elimu hiyo ameelewa jinsi anavyoweza kukuza uchumi kupitia ufugaji wa kisasa ambao una tija kubwa na ni rafiki kwa mazingira ya aina yeyote.









