“Yaani kinachoamua kiwango cha soka la nchi ni matokeo ya mechi za timu ya taifa?," aliuliza. “Mimi naona viwango vya Fifa havina maana kwa sababu haviangalii maeneo mengine muhimu ya kukuza soka kwenye nchi. Viwango hivi havionyeshi jinsi nchi inavyojitahidi kuboresha soka kuanzia ngazi za chini.
Kuna mambo mengi yanafanyika kukuza soka la nchi, lakini bahati mbaya ni kwamba viwango vya soka vya Fifa haviangalii mambo hayo," aliongeza.Alikosoa mfumo wa Fifa katika kuandaa viwango hivyo na kudai kuwa vina upungufu mwingi.
"Hawaangalii tangu chini jinsi soka linavyokuzwa. Kwa mfano, viwango vya Fifa haviangalii jinsi waamuzi wanavyofanya vizuri, jinsi viwango vyao vinavyoongezeka.
Fifa hawaangalii jinsi ligi zinavyoboreshwa na kuleta ushindani katika nchi. Kuna maeneo mengi ya soka katika nchi hii yameboreshwa kwa kiasi kikubwa. Haya ndiyo mafanikio ambayo Fifa wanapaswa kuyaangalia,” alisema Akinwunmi.
Alisema siyo sahihi kwa Fifa kuangalia mechi za timu za taifa kama kigezo cha kutathmini viwango vya ubora kwa mwezi.
“Hatutalala, tunafanya juhudi za kutosha kuwekeza nguvu nyingi katika soka kuanzia ngazi ya chini. Tuna malengo ya kuhakikisha soka letu linapanda kwa kiwango kikubwa lakini siyo kwa kuangalia viwango vya Fifa."










