Vita kali kabisa wiki hii

29Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Vita kali kabisa wiki hii

Ni kama bahati mbaya! Arsenal imepangwa dhidi ya Barcelona ya Hispania -- timu ambayo, hakuna timu nyingine zilizofuzu kwa hatua ya mtoano (16 - bora) Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyotaka kupangwa nayo.

WACHEZAJI WA ARSENAL

Ni kama bahati mbaya! Arsenal imepangwa dhidi ya Barcelona ya Hispania -- timu ambayo, hakuna timu nyingine zilizofuzu kwa hatua ya mtoano (16 - bora) Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyotaka kupangwa nayo.

Kupangwa na timu nyingine nje ya Barcelona ingekuwa nafuu, pengine nafuu na heri kucheza na Bayern Munich au Real Madrid kuliko Catalan.

Safu ya ushambuliaji bora kabisa kwa sasa Ulaya na duniani ya Barcelona inayoundwa na watatu kutoka mataifa ya Argentina, Uruguay na Brazil ndiyo tatizo kubwa.

Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar ni safu bora kuwahi kupatikana ndani ya kikosi hicho kwa miaka ya karibuni. Wachezaji hawa wamekuwa wakifunga mabao wanavyotaka, lakini kubwa linaloendelea kubaki swali lisilo na majibu ya haraka ni kwamba, ukuta wa Arsenal unaweza kuwazuia washambuliaji hawa?

Takwimu na kumbukumbu za nyuma za timu hizi katika mashindano haya, yanaipa nafasi kubwa Barcelona kuliko Arsenal.
Soka ni mchezo wa makosa, kama ilivyo jirani kwa safu ya Arsenal kufanya makosa mengi itakapojaribu kuwazuia Messi, Suarez na Neymar, ndivyo itakavyokuwa safu ya Barcelona.

Arsenal walimaliza Ligi ya Mabingwa Kundi F nyuma ya Bayern Munich, ni timu pekee sambamba na Real Madrid waliowahi kufika hatua ya mtoano wa michuano hiyo kila mwaka tangu mfumo mpya wa kuendesha mashindano hayo ulipoanza kutumika msimu wa mwaka 2003/04. Hata hivyo, hawajawahi kuvuka hatua ya mtoano 16 kwa misimu mitano mfululizo ya mwisho.

Barcelona waliomaliza Kundi F mbele ya Roma, wamecheza hatua ya mtoano kwa misimu 12 mfululizo.
Wanecheza hatua ya nusu fainali mara saba katika misimu nane. Ni msimu wa mwaka 2013/14 ndiyo waliondolewa kwenye hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Atletico Madrid.

Barcelona wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara nne katika misimu 10 ya mwisho. Hakuna klabu iliyowahi kutwaa taji zaidi ya mara moja katika kipindi hicho. Timu pekee kuwahi kufanya hivyo ni AC Milan ya Italia 1989/1990.