Twitter yatimiza miaka kumi

25Mar 2016
Restuta James
Nipashe
Twitter yatimiza miaka kumi

MTANDAO wa kijamii wa Twitter umetimiza miaka 10 tangu ulipoanza kutumika rasmi mwaka 2006.

nembo ya twitter.

Mtandao huo ambao una mamilioni ya watu ambao wametokea kuupenda na kuujua; na katika kutimiza miaka hiyo hauna mpango wa kuongeza tarakimu za uandishi wake kuzidi 140.

Biashara kubwa na ndogo ndogo zimejiunga na mtandao huo na kutoa maelezo mbalimbali kuhusu biashara zao.

Twitter pia umekuwa mtandao wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii, vuguvugu la nchi za kiarabu la mwaka 2011 liliutumia sana mtandao huu kupeana taarifa juu ya yale yaliokuwa yakiendelea.

Makao makuu ya mtandao wa Twitter yapo San Francisco na una ofisi zaidi ya 25 kwingineko duniani.

Twitter ilianzishwa Machi 2006 na Jack Dorsey, Evan Williams, Biz Stone na Noah Glass na kuzinduliwa Julai 2006.
Mtandao huo unatajwa kufahamika haraka duniani kote na hadi mwaka 2012 ulikuwa na watumiaji milioni 100 wanaoposti tweets milioni 340 kwa siku.

Mwaka 2013, Twitter ulitajwa kuwa miongoni mitandao 10 inayotembelewa zaidi duniani na Mei 2015, Twitter ilikuwa na zaidi ya watumiaji milioni 500 million.

Twitter inasimamiwa na Mwenyekiti ambaye ni Omid Kordestani na Ofisa Mtendaji Mkuu, Jack Dorsey.