Timu saba zinazoongoza mikataba minono ya jezi

29Aug 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
Timu saba zinazoongoza mikataba minono ya jezi

KLABU za soka ziliingia mikataba ya udhamini na chapa za nguo za michezo ili kuzalisha na kusambaza vifaa vya timu na bidhaa nyinginezo. Hiki ni chanzo kikubwa cha mapato kwa klabu za soka kwani mikataba hii inazisaidia kuzalisha kiasi kikubwa kupitia chapa na uuzaji.

 

Dili la jezi kwa kawaida huhusisha jezi za klabu, vifaa vya mazoezi, mavazi mengine na bidhaa mbalimbali za mashabiki. Jumla ambayo chapa inalipa kwa mpango kama huo inaweza kutofautiana kulingana na umaarufu wa klabu ulimwenguni na mafanikio yake.

Ofa za vifaa si tu huchangia uimara wa kifedha wa klabu, lakini huchangia katika kuunda utambulisho wake na utambuzi wa chapa. Hii ni kwa sababu muundo au mwonekano wa seti ya timu inakuwa sehemu muhimu ya uwakilishi wake wa kuona. 

Acha sasa tuangalie timu saba zilizo na ofa kubwa zaidi za jezi zinazolipwa kwa msimu...

                         

#7 Chelsea - Euro milioni 70 kwa msimu (Nike)

Chelsea ilitia saini mkataba wa jezi na miamba ya nguo za michezo ya Nike ambao ulianza kutekelezwa msimu wa 2017-18. Ndio mkataba mkubwa zaidi wa kibiashara katika historia ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England. Mkataba huo una thamani ya Euro milioni 70 kwa msimu na utaendelea kwa miaka 15 kutoka mwaka 2017.

Kabla ya kusaini mkataba huo, Chelsea ilipunguza mkataba wa Adidas uliokuwapo kwa miaka sita. Mkataba huo na kampuni ya Nike uliripotiwa kuongeza maradufu mapato ya 'The Blues' hao kutokana na makubaliano yao ya awali na Adidas.

 

#6 Manchester City – Euro milioni 75 kwa msimu (Puma)

Hili ndiyo dili pekee kati ya 10 zilizoingiza fedha nyingi zaidi duniani ambazo hazihusishi Adidas au Nike. Manchester City walitia saini mkataba huo mwaka 2019 na thamani yake ni Euro milioni 75 kwa msimu. Hata hivyo, kwa kuwa mkataba huo una miaka minne sasa na City ilishinda mataji matatu msimu uliopita, huenda ukaongezwa tena.

Mashabiki wa City wameonekana kufurahishwa na jezi ambazo Puma wameweka katika misimu ya hivi karibuni. Lakini wakati huo huo, kimekuwa kipindi kizuri cha mafanikio kwa City na mashabiki huwa hawalalamiki chochote wakati kabati ya vikombe inapokuwa imejaa.

 

#5 Paris Saint-Germain - Euro milioni 80 kwa msimu (Nike)

Umaarufu na mafanikio ya Paris Saint-Germain kwenye jukwaa la kimataifa, pamoja na kikosi chao chenye nyota wengi, uliwafanya kuwa mshirika muhimu wa Nike. PSG wameweza kusajili baadhi ya wanasoka bora duniani kama Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe katika miaka ya hivi karibuni.

Umaarufu wao katika kiwango cha kimataifa umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo uliopita na imekwenda mbali sana kuwasaidia kupata mkataba wa faida wa vifaa vya Nike.

 

#4 Arsenal – Euro milioni 85 kwa msimu (Adidas)

Adidas waliongeza mkataba wao wa jezi na Arsenal Septemba mwaka jana. Kwa mujibu wa makubaliano mapya, wataendelea kutengeneza na kusambaza vifaa vya 'Washikabunduki' hao hadi 2030. Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo mpya, Arsenal itaingiza euro milioni 85 kwa msimu kutoka Adidas.

Adidas na Arsenal zimeripotiwa kuangazia kuwekeza katika kutengeneza safu za bidhaa kwa wachezaji na mashabiki wa kandanda na pia kuwekeza katika jamii za wenyeji.

 

#3 Manchester United – Euro milioni 87.5 kwa msimu (Adidas)

Manchester United wameweka kalamu kwenye mkataba wa jezi kubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu England. Mkataba huo mpya utaendelea hadi mwaka 2035 na unawakilisha nyongeza ya miaka 10 kwenye makubaliano yao ya sasa na Adidas.

Kwa mujibu wa mkataba huo mpya, Manchester United itaingiza kiasi cha Euro milioni 87.5 kwa mwaka, na kuwafanya kuwa wanaolipwa fedha nyingi zaidi kupitia udhamini wa jezi kwenye Ligi Kuu England.

 

#2 Barcelona – Euro milioni 105 kwa msimu (Nike)

Nike imekuwa msambazaji rasmi wa jezi za Barcelona tangu mwaka 1998. Pande zote mbili zimeonesha nia ya kufanya kazi pamoja na hii imesaidia uhusiano wao kukua kwa miaka mingi. Mnamo 2018, Barca iliongeza mkataba wao na Nike kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa mkataba huo mpya, Barcelona wanapata euro milioni 105 kwa msimu kutoka kwa Nike. Ni dili la pili kwa bei ghali zaidi katika historia ya mchezo huo mzuri.

 

#1 Real Madrid – Euro milioni 120 kwa msimu (Adidas)

Kama vile Barcelona na Nike, Real Madrid na Adidas wamekuwa na ushirikiano tangu mwaka 1998. Ushirikiano huo unatazamiwa kuendelea hadi mwaka 2028 kulingana na masharti ya makubaliano yaliyokubaliwa kati ya pande hizo mbili mnamo mwaka 2019.

Real Madrid itapokea kitita cha Euro milioni 120 kwa msimu kutoka kwa Adidas na ni dili la jezi zenye faida kubwa zaidi katika historia ya soka.