Sababu 4 Pochettino kutafiti ukocha Chelsea

08May 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
Sababu 4 Pochettino kutafiti ukocha Chelsea

CHELSEA imeripotiwa kukaribia kumwajiri Mauricio Pochettino kama kocha wao mpya baada ya The Blues hao kuamua kumfukuza Graham Potter mwanzoni mwa Aprili. Umepita takribani mwaka mmoja tangu Todd Boehly & Clearlake Capital wachukue mikoba ya umiliki hapo Stamford Bridge, lakini haijapita miezi 12

 

 

Wamiliki hao walimfukuza Thomas Tuchel Septemba na kumwajiri Potter, na kumwachia aende miezi saba baadaye.

Frank Lampard ameajiriwa kama kocha wa muda, lakini klabu hiyo inahitaji mwelekeo mpya baada ya matumizi makubwa msimu huu. Kwa hiyo, kuajiriwa kwa Pochettino kunaweza kuwa uteuzi mzuri kwa Chelsea, haswa baada ya Julian Nagelsmann na Luis Enrique kuripotiwa kuwa nje ya kinyang’anyiro hicho.

Kwa maelezo hayo, hebu tuangalie sababu nne kwa nini Pochettino atafaa kuwa kocha pale Chelsea.

#4 Kukuza wachezaji wachanga

Tottenham Hotspur watakuwa na kumbukumbu nzuri za Pochettino na moja ya sababu kuu nyuma yake ni uwezo wake wa kukuza wachezaji wachanga.

Wachezaji watatu Dele Alli, Heung Min-Son na Harry Kane walistawi chini ya Muargentina huyo. Kieran Trippier pia aligeuzwa kuwa beki wa kulia wa kiwango cha kimataifa na kuchukua nafasi ya Kyle Walker. Kwa hiyo, hakika anajua njia ya kuwazunguka wachezaji wachanga, ambayo inaweza kuwa sababu kubwa nyuma ya Chelsea kumteua.

The Blues hao wametumia fedha nyingi katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, huku wachezaji 15 wakiongezwa kwenye kikosi na 11 kati yao wakiwa chini ya umri wa miaka 25. Mason Mount, Kai Havertz, Christian Pulisic, Armando Broja, Lewis Hall, Reece James, Conor. Gallagher, na Trevoh Chalobah pia wanaangukia katika mabano hayo ya umri.

Isitoshe, chipukizi Levi Colwill na Ian Maatsen, ni miongoni mwa wachezaji wengine waliotolewa kwa mkopo, wamevutia na wana uwezekano wa kutaka kupigania nafasi kwenye kikosi msimu ujao.

Kwa hiyo, kuna vipaji vingi vya vijana vya kuboresha na kukuza, licha ya ukweli kwamba kutakuwa na mauzo makubwa pia msimu huu wa joto. Pochettino inasemekana anataka The Blues kuangazia zaidi vipaji vya nyumbani, na hii ni ishara nzuri kwa klabu ambayo inataka kujenga kikosi cha vijana na wenye njaa ya kushinda mataji.

Uteuzi wake unaweza pia kumshawishi Mason Mount kusaini mkataba mpya, huku Pochettino akiripotiwa kuwa shabiki wa mchezaji huyo.

#3 Kuunda kikosi cha mafanikio

Ingawa Pochettino hakufurahia mafanikio makubwa katika klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), muda wake akiwa Tottenham Hotspur ulikuwa wa maana zaidi kwani alifuzu kwa kuwachomoa wachezaji bora zaidi kati ya waliokuwa na kiwango cha chini.

Wachezaji kama Moussa Dembele, Ben Davies, Harry Winks, Moussa Sissoko, na wengine wengi waliimarika sana wakati wa utawala wa Pochettino klabuni hapo.

Chelsea, kama Tottenham mwaka 2014, wana kikosi kichanga na nyota wenye uzoefu. Hata hivyo, ni kikosi ambacho hakina mafanikio makubwa, kutokana na vipaji vyao na uwezo wao na uchezaji katika klabu zao za awali.

Wachezaji kama Kai Havertz, Kalidou Koulibaly, Mykhailo Mudryk, Marc Cucurella, Hakim Ziyech, na Christian Pulisic wamekuwa chini ya viwango kwa muda wa miezi 12-18 iliyopita.

Lakini Pochettino bila shaka anaweza kubadilisha nguvu hii kwa kuunda mifumo unaowaruhusu kustawi.

Pia kuna suala la Romelu Lukaku, ambaye amekuwa na kipindi kizuri cha pili cha msimu akiwa kwa mkopo Inter Milan. Mbelgiji huyo alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu wakati huo ya pauni milioni 97.5 lakini alitolewa kwa mkopo msimu wa joto kufuatia msimu mbaya ndani na nje ya uwanja. Bado haijafahamika kama ana mustakabali ndani ya Chelsea, lakini kumtumia ipasavyo kunaweza kumpa Pochettino namba 9, kitu ambacho klabu hiyo inakihitaji sana.

Msimu wa sasa umeonyesha ukosefu wa matumizi sahihi ya vipaji katika klabu. Kwa hivyo, Pochettino anaweza kufanya moja ya malengo yake kuu ni kubadilisha hali ya wachezaji kama hao na kuwasaidia kutambua uwezo wao haraka iwezekanavyo.

#2 Uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu

Kazi ya mwisho ya usimamizi ya Pochettino inaweza kuwa Ufaransa, lakini sio siri kwamba moja ya nyakati zake nzuri zaidi kwenye ukocha ilikuwa miaka mitano pale London Kaskazini.

Tottenham ilimwajiri msimu wa joto wa 2014 baada ya mwaka mzuri sana kule Southampton. Katika misimu yake mitano, aliisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi nne za juu mara nne. Klabu hiyo ilimaliza katika nafasi nne za juu mara mbili tu ndani ya miaka 22 kabla ya kuteuliwa kwake. Kwa hiyo, hakika aliifanya Spurs kuwa na nguvu.

Kwa hiyo, Pochettino hakika anajua jinsi ya kuunda timu ambayo inaweza kushiriki kikamilifu katika Ligi Kuu, jambo ambalo limekuwa baya pale Stamford Bridge msimu huu. The Blues hao hawajashinda taji la ligi tangu mwaka 2017 na tangu wakati huo pia hawajawa kuwa katika mbio za kuwania, huku Manchester City na Liverpool zikitawala.

Maurizio Sarri, Frank Lampard, na Thomas Tuchel walijaribu kubadilisha simulizi hiyo, lakini walishindwa au hawakuweza kudumisha changamoto ya ubingwa kwa zaidi ya miezi sita.

Timu za Pochettino ni endelevu zaidi, ingawa hakuzungusha kikosi chake vya kutosha pale Tottenham. Lakini Chelsea hakika wana kikosi chenye kina na chenye uwezo wa kufanya kazi nacho na kocha huyo wa Amerika Kusini anaweza kuwasaidia kuwa thabiti zaidi kwenye ligi. Kurejea kwenye nafasi nne za juu itakuwa moja ya vipaumbele vyake.

#1 Mbinu katika michezo mikubwa

Pochettino, wakati wa Espanyol, Southampton, Tottenham, na PSG, hakuwahi kutawala mechi dhidi ya timu yoyote kubwa.

Hata hivyo, ni vyema kutambua kwamba, ukiondoa PSG, hakuna timu yake iliyowahi kushinda mataji au kuwa na timu ya viongozi. Lakini Pochettino alikuwa na njia yake ya kuzichambua timu zake na moja ya ishara za kwanza za ustadi wake wa kimbinu ilikuwa ushindi wa Espanyol wa 2-1 ugenini dhidi ya Barcelona ya Pep Guardiola mnamo 2009.

Ingawa hakuweza kamwe kuangusha timu yoyote ya juu akiwa na Southampton, maonesho yalikuwa ya kutia moyo. Hata hivyo, wakati alipokuwa Tottenham, rekodi ya Pochettino iliboreka kidogo, kama inavyopaswa kuwa.

Wakati wa kukutana mara 10 na Arsenal kama kocha wa Spurs, walishinda mara nne na kuandikisha sare mbili. Alikuwa na rekodi sawa dhidi ya Chelsea na pia aliandikisha ushindi mara nne katika mechi 10 dhidi ya Manchester United. Ingawa kiwango cha timu yake dhidi ya Liverpool na Man City hakikuwa kizuri sana, alimshinda Guardiola kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mechi mbili za msimu wa 2018/19.

Lakini mbinu za Pochettino ni nzuri na zenye nidhamu ya ajabu. Ana ubora wa kuongeza mabeki wake wa pembeni na kuipa ulinzi uhuru kidogo. Vile vile, anaweza kufundisha uchezaji wa ushambuliaji thabiti na mzuri ilhali safu yake ya kati inaweza kuwa mbunifu na pia kufanya kazi kwa uharaka.

Ni mtu anayeongozwa na kanuni badala ya mifumo na anaweza kuzoea kikosi badala ya kununua wachezaji wanaoendana na aina yake ya uchezaji. Hiki ndicho ambacho Chelsea wanakihitaji kwa sasa kwani kuongeza fedha nyingi msimu wa joto tena haiwezekani.