Hata hivyo, mafanikio yao yametokana na makocha wao wa hali ya juu, ambao si tu kwamba wamebadili falsafa katika klabu hiyo, lakini pia wamejenga tabia na molari ya ushindi.
Makocha ndio uti wa mgongo wa klabu yoyote, na mafanikio ya msimu huanza na kumalizika nao. Hata hivyo, kumekuwa na baadhi ya makocha katika misimu ya hivi karibuni ambao wamekuwa wakibezwa sana.
Lakini kuna wachache ambao wamethibitisha uwezo wao kwa usimamizi na ujuzi wa kimbinu msimu huu.
Kwa maelezo haya, sasa tuwaangalie makocha watano ambao wamewanyamazisha wale wote waliokuwa wanawabeza msimu huu...
#5 Unai Emery - Aston Villa
Msimu wa Aston Villa 2022/23, umekuwa chini ya rada, huku klabu hiyo kutoka Jiji la Birmingham ikiwa katika mbio za kufuzu kuwania kucheza Ligi ya Europa msimu ujao.
Baada ya kuambulia pointi tisa pekee katika michezo 11 ya kwanza ya Ligi Kuu, timu hiyo ilifikisha alama 41 katika michezo 22. Sasa wapo katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa mashindano ya Ulaya msimu ujao. Lakini kuibuka upya kumekuwa chini ya Unai Emery, ambaye aliondoka Villarreal na kujiunga na Villa Novemba mwaka jana.
Emery anafahamu wazi jinsi timu zake zinapaswa kucheza. Ingawa inahitaji mbinu makini, bosi huyo wa Hispania ameweza kuweka hali ya nidhamu katika timu ambayo ilikuwa kwenye hali ngumu chini ya Gerrard.
Ollie Watkins amecheza mbele kwa kujitolea na kufunga mabao 14 ya ligi msimu huu. Jacob Ramsey amekua na kipaji kizuri, wakati wachezaji kama Ezri Konsa, Douglas Luiz, Emiliano Martinez, na John McGinn wametoa msingi mzuri kwa upande mwingine. Kwa hiyo kila mchezaji anacheza kwa uwezo wake, shukrani kwa mfumo mzuri uliotumiwa na Emery.
Mhispania huyo atafurahishwa na timu yake, haswa baada ya mbinu zake kukosolewa na mashabiki kadhaa wa Arsenal wakati alipokuwa kule Emirates. Lakini tangu wakati huo, Emery amejidhihirisha akiwa Villarreal na sasa amerejea Ligi Kuu England na kuwaziba mdomo wale wote waliombeza.
#4 Eddie Howe - Newcastle United
Utajiri wa Newcastle United ulilazimika kubadilika mara tu baada ya kuchukuliwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma (hazina ya utajiri wa nchi ya Saudi Arabia).
Lakini ni wachache waliotarajia klabu hiyo kuwania nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa haraka sana. Shukrani kwa Eddie Howe, nyakati nzuri zimerejea, wameamka na wananguruma tena.
Ingawa sera yao ya kuajiri imekuwa nzuri, kocha huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 45, amekuwa sababu kuu ya maendeleo makubwa ya klabu hadi sasa.
Wakati alipokuwa Bournemouth, mbinu za kushambulia za Howe zilisifiwa mara kwa mara. Hata hivyo, amepata uwiano sawa Newcastle, na timu kuwa na ulinzi thabiti na nguvu ya kusisimua ya kushambulia.
Kuongezwa kwa Bruno Guimaraes, Dan Burn, Alexander Isak, Nick Pope, na wengine kadhaa katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, kumechangia kwa kiasi kikubwa kwenye hili. Kuibuka tena kwa wachezaji kama Miguel Almiron na Joe Willock pia kumekuwa ufunguo wa maendeleo ya klabu msimu huu.
Huku timu hiyo ikishika nafasi ya nne kwenye jedwali zikiwa zimesalia mechi nane pekee msimu kukamilika, Howe amethibitisha ubora wake katika soka la England msimu huu.
#3 Xavi Hernandez - Barcelona
Xavi Hernandez ameleta mapinduzi makubwa katika Klabu ya Barcelona msimu huu, hasa baada ya kushindwa kushinda taji la Ligi Kuu Hispania, LaLiga, katika misimu minne iliyopita. Lakini mambo yamebadilika sasa. 'Blaugrana' hao wametawala takriban kila mechi za ligi msimu huu na inastahili pointi 11 mbele ya Real Madrid iliyo nafasi ya 2 kwa sasa.
Hili limewezekana tu kutokana na mabadiliko ya mbinu ya Xavi, huku kocha huyo akitanguliza ubabe katika safu ya kiungo. Mara nyingi amechagua kuwapanga viungo wanne kati ya Frenkie de Jong, Sergio Busquets, Franck Kessie, Gavi, Pedri, na Sergi Roberto.
Hii imewawezesha kutawala mpira katika michezo mingi, huku wachezaji kama Ousmane Dembele, Raphinha, na Robert Lewandowski wakiwa wamejiweka sawa mbele ya lango.
Safu ya ulinzi pia imepangwa, huku Ronald Araujo akicheza nafasi ya nyota nyuma msimu huu. Ameongoza safu ya ulinzi kwa ustadi, na kuibuka kwa Alejandro Balde katika beki wa kushoto pia imekuwa nyongeza nzuri.
Wakosoaji wengi walitilia shaka sifa za usimamizi za Xavi wakati wa uteuzi wake kwani hapo awali alikuwa ameiongoza Al Sadd nchini Qatar. Hata hivyo, hatimaye amekuwa mzuri kwa klabu yake ya utotoni na atatafuta kuipeleka Barcelona kileleni mwa mashindano ya Ulaya msimu ujao.
#2 Jose Mourinho - AS Roma
Jose Mourinho bila shaka ndiye kocha mkuu zaidi wa karne ya 21, mataji na sifa zake zinajulikana wazi.
Tangu alipowasili kwenye eneo la tukio baada ya kuiwezesha FC Porto kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2004, bosi huyo wa Ureno hajageuka nyuma. Alifanya vema akiwa Chelsea kwa kutwaa mataji mawili huku pia akishinda mataji matatu akiwa na Inter Milan. Muda wake akiwa Real Madrid pia ulikuwa wa kustaajabisha, ingawa hakuweza kushinda Kombe la Ulaya akiwa nao.
Hata hivyo, alipokea shutuma nyingi kwa mbinu zake za kizamani za ulinzi wa "kupaki basi" wakati alipokuwa Manchester United na Tottenham Hotspur. Kwa hiyo, wachache walitarajia mzee huyo wa miaka 60, asingerejea kwenye ubora, lakini Mourinho amefanya hivyo. Tangu achukue mikoba ya AS Roma msimu wa majira ya joto wa 2021, ameleta mabadiliko katika klabu hiyo.
Nyongeza za Tammy Abraham, Roger Ibanez, Paulo Dybala, Nemanja Matic, na wengine kadhaa zimeleta uthabiti na ustadi wa kushinda michezo. Mbinu yao ya kushambulia imekuwa ya moja kwa moja zaidi, na safu yao ya ulinzi ni ngumu sana, na kuwafanya kuwa timu ngumu kucheza dhidi yao.
Sifa hizi ziliwafanya kushinda Kombe la Ligi ya Europa Conference mwaka jana, na kwa sasa wako nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A. Timu hiyo ya Italia haijashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu msimu wa 2018-19, jambo ambalo Mourinho amekuwa akitaka kulibadilisha tangu achukue nafasi hiyo.
Mbinu za bosi huyo wa Ureno zinaweza kuwa za kisayansi kidogo kwenye Ligi Kuu, lakini kwa hakika amevunja kanuni tena katika soka la Italia. Mtu maarufu kwa kupata mambo makubwa akiwa na watu wa chini, Mourinho hakika bado ni mmoja wa makocha bora katika soka la dunia.
#1 Mikel Arteta - Arsenal
Ikiwa kuna timu moja katika soka ya dunia ambayo imefanya zaidi ya matarajio yote msimu huu, hakika ni vijana wa Mikel Arteta, Arsenal.
Wakati Edu na Arteta wamekuwa wakijenga mradi huu kwa uthabiti na kwa busara katika miaka miwili iliyopita, kazi yao imeleta mafanikio katika msimu wa sasa. Tangu siku ya kwanza ya msimu wa 2022-23, Arsenal imekuwa na hali ya ndani ya kujiamini, nia na molari ya kuzishinda timu pinzani.
Wachezaji kama Bukayo Saka, Martin Odegaard, Oleksandr Zinchenko, Granit Xhaka, na Aaron Ramsdale wametoa msingi kwa timu kwa kutoa maonesho ya 9/10 wiki baada ya wiki.
Kuongezwa kwa Gabriel Jesus na Zinchenko majira ya joto, pamoja na kuwasili kwa Jorginho na Leandro Trossard, pia kumeiwezesha Arsenal kuendeleza changamoto ya ubingwa.
Lakini hakuna hata moja ya mambo haya ambayo yangewezekana bila mbinu za Arteta. Mhispania huyo amehimiza timu yake kuwa na jeuri zaidi, hesabu, molari na busara katika maeneo yote ya uwanja. Iwe kupitia pasi za haraka, za kusisimua kati ya mistari au kuwafundisha mawinga wake jinsi ya kupokea mpira, mfumo wa Arteta umekuwa usio na dosari.
Kitu ambacho pia amefanikiwa kukimiliki ni kutengeneza safu ya ulinzi inayojiamini na bila mpira na haina hofu ya kucheza safu ya juu. Kwa mtu ambaye alikosolewa vikali hadi mwisho wa msimu uliopita, Arteta hakika amewanyamazisha wapinzani wake msimu huu, jambo ambalo bila shaka anaweza kujivunia.










