Akerwa uharibifu mazingira, anuia kupanda miti milioni tano kijijini

29Dec 2022
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Akerwa uharibifu mazingira, anuia kupanda miti milioni tano kijijini
  • Kila mwezi 2,700; azama mfukoni Mil. 11/-

NI kwamba ameamua kujitosa kuimaliza kazia kuwa mwanamazingira wa ukweli, tena kwa vitendo, Adama Diémé (48), mwanaume raia wa Senegal, amejiwekea dhamira kupanda miti milioni tano katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

• Adama Diémé (kushoto), akiwa kijijini kwao na mbegu ya miche ya miti anayotarajia kuipanda. Fulana aliyovaa ni sare ya kampeni hiyo aliyobuni kutumia mafundi cherehani kijijini kwao. PICHA: MTANDAO

 

Kwa lugha rahisi ni ajenda ya kupanda miti milioni moja kila mwaka, au kila mwezi miti 2,740, hali kadhalika wastani wa miti isiyopungua 90 kila siku.

Ni wazo la mradi uliomjia pale aliporudi nyumbani eneo la Casamance mwaka 2020, baada ya kufanya kazi barani Ulaya.

Mwanaume huyo alishangaa kwamba vijiji ambavyo vilikuwa na mamia ya miti mikubwa katika ujana wake, ni michache tu sasa imebaki, ikamuuma sana.

Katika baadhi ya vijiji analaumu mtu hawezi kupanda hata mti mmoja, akilalamika wanakata, lakini hawafikirii kuupanda tena. Ni kilio anachosema kinatawala Afrika nzima haya kushuhudiwa jangwa.

Anasema, kando ya eneo kubwa la Mto Casamance, miti hiyo ina uwezekano mkubwa wa kukatwa kwa madhumuni ya ujenzi kama vile nyumba, au kuchoma mkaa.

Diémé, ambaye sasa ni Meneja wa Mradi katika shirika lisilo la kiserikali la huko kwao, huku akiwa mzalendo anayejitolea ukufunzi wa kilimo kwa kinamama kijijini, ameazimia kubadilisha hali aliyoikuta.

Akiwa hana akiba kubwa ya mali, anasema alianza kuchangisha pesa ili kutimiza ndoto yake na ametumia Dola za Marekani (Sh. milioni 11.750) za kutoka mfukoni mwake kuanzisha mpango huo.

Amekuwa akifanya kazi kwa kushirikiana na jamii zinazomzunguka kufikia wanawake ambao alijua wangeweza kumsaidia kuandaa upandaji kwa wingi miche.

"Unaenda katika kijiji na hakuna wanawake, ni janga," Diémé analalamika akiendelea:"Lakini ukienda kwenye kijiji chenye wanawake pekee, ni paradiso  wanafanya kazi kwa bidii na wanafanya kazi siku nzima kila siku. Ikiwa unataka kuongoza mradi mzuri anza na wanawake.”

Alichokifanya ni kuunganisha mradi wake wa kupanda miti kwa kuwasaidia wanawake kupata ujuzi wa kuwa wakulima wadogo na kuuza mazao yao katika masoko ya ndani.

"Mwanzoni, hatukujua jinsi ya kupanda mbegu na nini cha kufanya ili kukuza mazao," mmoja wa wanawake, Safi Yetou, anamsifu.

"Sasa tuna kila aina ya matunda ya kuuza sokoni na hatumtegemei mtu yeyote. Sote tuna akaunti katika benki sasa na hakuna mtu anayeweza kuniambia ninachoweza au nisichoweza kufanya. Ni vizuri."

Mradi huo wa Diémé unajulikana kama Ununukolaal, jina ambalo katika lugha ya kienyeji linamaanisha "Miti Yetu".

Kuna aina 12 ya miti inayopandwa ikiwamo mitende na limao, kutegemea na  hali ya ardhi na mahitaji ya jamii. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, alishapanda zaidi ya miche 142,000 imetunzwa na kuota mizizi.

Mshirika wake, Yolanda Pereñiguez, anayefanya kazi ya ufundi cherehani kijijini, amekuwa muhimu katika kusaidia kupanga fedha kwa kubuni fulana inayouzwa nje ya nchi kwa  dola 15 (Sh. 35,000), akiwa na Raymonde Coly, anayefanya kazi katika karakana ndogo yenye cherehani mbili ili kuzitengeneza kutoka kwa nguo za kienyeji, zenye picha ya kipekee ya mbuyu. Kila moja inayouzwa inaweza kulipia miche 15 ya miti.

"Nilichagua mbuyu kwani ni alama ya mti wa Kiafrika," anasema  Periniguiz, akifafanua: “Inapendeza kujua kwamba fulana hizi zinakwenda duniani kote, Ulaya na hata Canada kusaidia mradi wa miti."

Miaka 10 iliyopita, viwango vya ukingo wa maji ulikuwa mbali zaidi na kufika kijijini hapo ambako ni kisiwa, isipokuwa katika kilele cha msimu wa mvua. Sasa ni hali ya kukata tamaa na ikiwa inaweza kumaanisha kuwaacha wakazi bila makazi.

"Tumeishi katika kisiwa hiki kwa mamia ya miaka, lakini kama maji yanakuja zaidi tutalazimika kuondoka na kutawanyika kila mahali," Conakry Bassene, kiongozi wa kijiji.

Miti ya mbuyu, ambayo inaweza kuishi ardhini na kwenye maji yenye chumvi au majisafi, sasa imepandwa kando ya ufuo kama kizuizi. Miche hupiga upepo, kwa ahadi ya matunda siku moja  na hata kivuli. Miti inaweza kutuokoa," anasema Bassenem, akifafanua "Miti, ndio tumaini letu la maisha."