Katika ujumbe wake, Rais Xi alidokeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, AU imeungana na kuziongoza nchi za Afrika kutatua kikamilifu changamoto za kimataifa, kuharakisha ujenzi wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na kuwa na nafasi muhimu katika upatanishi wa masuala ya mizozo.
Aliongeza kuwa hadhi ya kimataifa na ushawishi wa Afrika umeendelea kuongezeka.
“Ninazitakia kwa dhati nchi za Afrika na watu mafanikio makubwa katika kuelekea kwenye maendeleo na ufufuaji," alisema Xi.
Rais wa China amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Afrika umedumisha kasi nzuri ya maendeleo mwaka 2022 kwani ushirikiano kati ya China na Afrika umeendelea kustawi kwa pande zote, ngazi mbalimbali na ubora wa hali ya juu na iko mstari wa mbele katika ushirikiano wa kimataifa na Afrika.
Xi amesema yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa Afrika ili kuimarisha zaidi urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika, kuratibu na kushirikiana kwa karibu katika masuala ya kimataifa na kikanda na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
(Chanzo: CGTN)










