Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Athumani Amasi, amesema kati ya watahiniwa hao wavulana ni 247,131 sawa na asilimia 46.19 na huku wasichana wakiwa 287,870 sawa na asilimia 53.81.
Amas amesema kati ya hao watahiniwa 533,001 wanatoka shuleni na wengine 31,839 ni wa kujitegemea, amesema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwemo mitihani kufika kwenye mikoa na vituo husika.
Amasi amesema katika idadi hiyo wapo watahiniwa wenye mahitaji maalumu 852 kati ya 480 wana uhoni hafifu, 62 wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia, 152 wenye mtindio wa akili na 139 wana ulemavu wa viungo.
"Mwaka 2021 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 538,024 hivyo kuja ongezeko la jumla ya watahiniwa 28,816 sawa na asilimia 5.36 kwa mwaka 2022 ukilinganisha na mwaka 2021.
"Maandalizi ya mtihani huu wa kesho yamekamilika ikiwa ni pamoja kusambazwa kwa mtihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani katika mikoa ya Tanzania na Zanzibar," amesema Amasi.










