Ombi hilo, lilitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassani, katika hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi iliyo andaliwa na jumuiya hiyo.
Hafla hiyo hiyo iliyofanyika jana jijin Dar es Salaam, ilihudhuriuwa na madhehebu mengine ya dini na viongozi mbalimbali wa serikali.
Masauni alisema, baada ya kutoa ombi hilo liliitikiwa kwa shangwe na kwamba ana uhakika litafanyiwa kazi kwa kuwa limetoka kwa mkuu wa nchi.
“Ninawapongeza sana Jumuiya ya Ismaili kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad, lakini nimeona mchanganyiko wa madhehebu mbalimbali hii inaashiria kwa vitendo ile sera ya umoja msihikamano na upendo baina ya watanzania wenye Imani tofauti, kabila na asili.
“Tunatambua kazi nzuri wanazozifanya kwa kutoa kutoa mchango mkubwa katika sekta ya afya, elimu uchumi, ninyi ni mashahidi juu ya huduma nzuri ya afya zinazotolewa na hospitali mfano ile ya Aghakani inasifika kwa huduma nzuri” alisema Muhandisi Masauni
Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Aga Khan Development Network nchini (AKDN), Amin Kurji, alisema watalifanyia kazi ombi la serikali la kushusha gharama za matibabu huku akiwasistiza watanzania kuitikia wito wa serikali wa bima ya afya kwa wote.
Alisema ili uweze kupata matibabu mazuri lazima uwe na bima ya afya, itakayo kusaidia kumudu gharama za matibabu na kwamba mpango wa bima ya afaya kwa wote utawasaidia watanzania wengi kupata matibabu bora yenye gharama za juu.
“Na sio tu kwa hospitali za Aga khan bali hata kwa zahanati nyingine, lakini kuhusu ombi la serikali tutaangali, vituo vyetu vya afya vipo 36 nchi nzima hii ya Aga khan ni kama ya rufaa lazima upitie huko halafu ndio wakulete hapa kwa hiyo tutaona nini cha kufanya” alisema
Kiongozi huyo alisema sherehe hiyo ililenga kusistiza thamani za kibinadamu kama vile huruma, uvumilivu, umoja, na juhudi za maendeleo ya binadamu, kulingana na mafundisho ya Nabii.









