Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya KIBAFA,Mabel Nasua amesema uchaguzi huo ulifuata taratibu zote za kisheria na kumtangaza Munis kuwa ndiye mwenyekiti wa chama hicho.
Munis,ambaye alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo alialishinda, kwa kupata kura 30 za ndio na moja ya hapana kati ya wapiga kura 31, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na David Mramba aliyepata kura 27, huku Katibu akiwa ni Daud Mhina aliyepata kura 29 na katibu msaidizi ni Omary Pumzi aliyepata kura 28.
Nafasi ya mweka hazina ilikwenda kwa Laurent Shirima aliyepata kura 28, mjumbe wa mkutano mkuu kwenda Corefa ni Japhet Mbogo aliyepata kura 30 na Mwakilishi wa vilabu Mohamed Mwenda aliyepata kura 28 Mwakilishi wanawake ni Jesca SihaKamati ya utendaji wakiingia Method Mselewa, Nasoro Shomvi na Emanuel Mbunda.
Akizungumzia mikakati yake katika kipindi cha miaka minne Munis amesema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha Kibaha inakuwa na timu ya ligi kuu ambapo ataweka mikakati Ruvu Shooting irudi kwenye ligi hiyo baada ya kushuka daraja.
Munis amesema kuwa atahakikisha mpira wa miguu unachezwa na kupata viwanja vizuri ili kukuza vipaji vya vijana kwenye soka ili waje kuwa hazina kwa timu za mkoa na taifa kwa ujumla.
Naye Katibu wa chama cha soka Mkoa wa Pwani COREFA Mohamed Masenga alisema kuwa kwa vyama ambavyo havijafanya chaguzi vifanye hivyo ili kwendana na kalenda ya vyama vikuu vya soka.
Kwa upande wake ofisa michezo wa Halmashauri ya Mji Kibaha Burhan Tulusubya amesema kuwa uchaguzi huo ulienda vizuri kwa kuzingatia taratibu za chama hicho na sheria kwani ulikuwa wa kisheria.










