Mdau wa maendeleo kuchangia ujenzi wa bweni shule ya Mahida

23Oct 2022
Anjela Mhando
Rombo
Nipashe Jumapili
Mdau wa maendeleo kuchangia ujenzi wa bweni shule ya Mahida

MDAU wa Maendeleo ambaye ni mzawa wa kijiji cha Mahida Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro Wakili Anthon Mseke amechangia kiasi cha Sh milioni 4 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari ya Mahida iliyo wilayani hapo lengo likiwa kukamilika kwa bweni hilo.

Mgeni rasmi katika mahafali ya 24 katika shule ya Sekondari Mahida Wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro Wakili Anthony Mseke akizungumza na wazazi na wanafunzi (hawapo pichani) katika mahafali iliyofanyika shuleni hapo.

Mdau huyo amechangia fedha hizo leo kwa kukabidhi hundi ya Sh. milioni tatu na nusu huku akieleza laki tano inafuata siku chache zijazo katika mahafali ya 24 ya kidato cha nne iliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Mahida.

"Nikiwa kama mwanakijiji na mzawa wa eneo hili nimewiwa kutafuta marafiki zangu kule ninapoishi kwa sasa wakanichangia kiasi hicho kidogo ambacho nimewasilisha leo katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia mitihani yao , rai yangu kwa wanajamii na wadau wengine wa elimu waweze kuchangia ujenzi wa bweni hilo" amesema Mseke.

Aidha, amesema suala kuchangia Maendeleo ya elimu sio swala mtu mmoja bali ni suala la wananchi wote, tukiunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha kwamba elimu ina songa mbele,ambapo amesema maendeleo hayawezi kuletwa na serikali peke yake ,Serikali ni sisi ,na sisi ndio wahitaji wa maendeleo ,serikali ina mambo mengi inafanya tunahitaji kuunga mkono kuhakikisha kwamba na matatizo yote tunajaribu na sisi kuyatatua wananchi wote kwa pamoja bila kujali hali ya kipato ,suala la elimu afya ,na matatizo mengine ya kijamii ni suala la wote. ili tuweze kuendelea mbele kama Taifa tunahitaji ushiriki wa Mona kwa Moja kwa kila mwananchi bila kubagua.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Elifariji Meraro aamesema ujenzi wa bweni hilo umefika hatua za mwisho ambapo wamekuwa wakipata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na Serikali ambapo kwa mwaka huku 2022walipata sh.milioni mbili walizofanyia shughuli mbalimbali,ambapo kwa sasa bweni hilo linahitaji kumaliziwa kwa maana ya rangi,vitanda 22,tenki kwaajili ya kuhifadhia maji ,ambapo alisema bweni hilo linauwezo wa kuchukua wanafunzi 114 kwa wakati mmoja.

Diwani wa kata hiyo Issack Tarimo akizungumza ujenzi wa bweni hilo amesema amekuwa akienda maeneo mbalimbali kwa wadau wa maendeleo kwaajili ya kuhakikisha ujenzi unaendelea ,ambapo nilimtafuta mgeni rasmi huyu aliyekuja leo na alipofika ameweza kutoa milioni nne .

"Bweni hili hadi likamilike linahitaji zaidi ya shilingi milioni nane, hivyo kwa kiasi kilichopatikana leo bweni hili litasonga mbele ,ambapo amesema bado ataendelea kutafuta wadau ili kuweza kukamilisha ujenzi kwa haraka kwasababu kazi ya kiongozi wa kisiasa ni kusukuma maendeleoo,na kusukuma maendeleo ni kutafuta wadau mbalimbali wa maendeleo ili kazi ziende kwa kusaidiana na Serikali.