Mama aua watoto wake kwa sumu

10Mar 2024
Na Mwandishi Wetu
Mbeya
Nipashe Jumapili
Mama aua watoto wake kwa sumu

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia Daines Mwashambo (30) mkazi wa kijiji cha mashese Mbeya vijijini, kwa tuhuma za kuua Watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu ya kuulia magugu shambani.

Inadaiwa Daines alifanya tukio hilo akiwa nyumbani kwake lakini vifo vya watoto hao vilitokea muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP- Benjamini Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na Daines kutuhumiwa na Serikali ya Kijiji hicho kufanya udokozi na wizi kwa kuingia katika nyumba za watu.

Imeelezwa kuwa baada ya kuwanywesha sumu watoto wake, mtuhumiwa naye alikunywa sumu lakini akawaiwa kabla haijamuua ambapo kwasasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya chini ya ulinzi wa Polisi.