Madereva wa treni nchini Ujerumani wagoma tena leo

12Mar 2024
Ujerumani
Nipashe
Madereva wa treni nchini Ujerumani wagoma tena leo

MADEREVA wa treni wa shirika la reli nchini Ujerumani Deutsche Bahn, kwa mara nyingine leo hii wanaendelea na mgomo wao wa kushinikiza maslahi bora.

Hatua hiyo ni baada ya hatua ya shirika hilo kwenda mahakamani kuzuia mgomo huo, kwa kile ilichosema ni kinyume cha sheria na hivyo kusubirishwa.

Msemaji wa shirika hilo la reli, amethibitisha kuwa mgomo wa usafirishaji wa abiria unatarajiwa kuanza Asubuhi hii ya Jumanne na unatarajiwa kudumu kwa masaa 24.

Shirika hilo limepanga ratiba ya mkutano wa dharura kwa lengo la kufanikisha usafirishaji wa japo asilimia 50 ya safari za treni za masafa marefu. Huduma za safari za mji mmoja hadi mwingie na zile za vitongoji nazo pia zimeathirika.

Rufaa hiyo ya shirika la reli Deutsche Bahn haitasikilizwa hadi karibu na adhuhuri ya leo. Na Ikiwa Mahakama ya Kazi ya Jimbo la Hesse itatoa uamuzi tofauti na Mahakama ya Kazi ya Frankfurt, Chama cha Madereva wa Treni GDL kitalazimika kusitisha mgomo wake. Hata hivyo hatua hiyo haimaanishi kurejea kwa mara moja kwa huduma za kawaida usafirishaji.