Deby Itno alichukuwa madaraka mwaka 2021 baada ya baba yake, kiongozi mkongwe Idriss Deby Itno, kufariki wakati akipambana na waasi.
Kiongozi huyo alietawala kwa mkono wa chuma alikuwa ameiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miongo mitatu. Deby Itno alitangazwa kuwa rais wa mpito na uongozi wa kijeshi na aliahidi kurejesha utawala wa kiraia na uchaguzi katika kipindi cha miezi 18.
Lakini aliongeza kipindi cha mpito kwa miaka miwili. Tarehe ya uchaguzi ilitangazwa siku ya Jumanne, chini ya miezi miwili kabla ya kura.
Deby Itno mwenye umri wa miaka 39 ana uhakika wa kushinda kutokana mpinzani wake mkuu Yaya Dillo Djeru kuuawa siku ya Jumatano, na upinzani kukandamizwa.