Elia na wenzake 16 mbaroni kwa utapeli mtandaoni

08Mar 2024
Na Mwandishi Wetu
Morogoro
Nipashe
Elia na wenzake 16 mbaroni kwa utapeli mtandaoni

JESHI la Polisi mkoani Morogoro, wanamshikilia Elia Sidame mkazi wa Azimio Manispaa ya Morogoro na wenzake 16 kwa tuhuma za kufanya biashara hewa mtandaoni na kuwatapeli watu mbalimbali fedha zao na kuzua taharuki kwenye jamii.

Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Polisi (SACP), Alex Mkama.

Kamanada wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Polisi (SACP), Alex Mkama, amesema Sidame na wenzake wamekuwa wakitumia mbinu ya kuwarubuni watu kujiunga na kampuni hewa za mtandaoni na kuwatoza hela kuanzia shilingi milioni mbili na nusu na kuendelea kwa lengo la kupata faida kubwa.

Aidha, Kamanda Mkama amesema upelelezi wa matukio hayo unaendelea ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani huku akitoa onyo kwa wahalifu kuacha vitendo hivyo na endapo wataendelea hawatatoka salama katika mkoa wa Morogoro.