‘Ushuhuda’ ni album yenye mkusanyiko wa nyimbo 12 za kiroho zilizotengenezwa kwa ustadi na ufundi mkubwa na msanii huyo akishirikiana na baadhi ya maproduzya wa hapa nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Walter aliweza kumshukuru Mungu sambamba na mashabiki zake kwa kuandika “Sijui nisemeje jamani ni wiki tu sasa lakini mapokezi ya hii album yamekuwa makubwa sanaaa tumefika streaming laki tano (500K )chiiiii hakika namtukuza Mungu juu ya hili sifa kwa Yesu,,,,,,,Mungu awabariki sanaaaaaa hii inanipa nguvu Sanaa”.
Walter ameitaja albumu hiyo kuwa ni albumu bora kwani ameifanya kwa ubunifu na uwekezaji mkubwa na kuwataka mashabiki zake kuendelea kusikiliza na kupakua baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo. “Ushuhuda” ni album ya pili ya Walter baada ya ile ya kwanza ya ‘Asante’ ambayo ilitoka mwaka 2018.
Aidha, kupitia Album hii, Walter aliona haja ya kufanya kitu cha tofauti na wasanii wengine ambapo ameweza kuiandaa album hii katika ladha/miondoko tofauti ya muziki ikiwemo; - RnB, Amapiano, Afrobeats na Zouk.
Kitu cha kuvutia zaidi ni kuwa album nzima imetayarishwa na msanii mwenyewe akisaidiwa na Abydad na Criso Cris ambao walihusika kwenye hatua za mwisho za utayarishaji (mastering).
Walter anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao wameachia albamu/EP kwa mwaka huu kupitia jukwaa namba moja la kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay. Wengine ni pamoja na Meja Kunta, ambaye aliachia ‘Meja Power’ na Beka Flavour ambaye ameachia ‘First Born’ hivi karibuni.
Unaweza kuisikiliza na kupakua albamu ya Walter Chilambo bure kupitia linki ya Boomplay hapa:- https://www.boomplay.com/albums/46057774?from=search










