Ray alisema kuwa tangu atoe ufafanuzi huo baada ya 'kushambuliwa' katika wimbo wa 'Shika Adabu Yako' ulioimbwa na Nay wa Mitego kwamba anatumia fedha nyingi kununua vipodozi, anafikiria kufanya mazungumzo na makampuni yanayouza maji ili aweze kuwatangazia biashara hiyo.
"Ninaweza kwenda kampuni yoyote kuomba udhamini nikapata ama kutengeneza makala ya umuhimu wa maji nikapeleka kwenye vituo vya televisheni nikapata fedha, hii itakuwa ni utambulisho wangu pia,"










