Nay wa Mitego hayumbishwi

01Mar 2016
Sabato Kasika
Nipashe
Nay wa Mitego hayumbishwi

LICHA ya kukunbwa na misukosuko ikiwamo ya gari lake kupopotewa mawe, rapa Nay wa Mitego amesema hatarudi nyuma kuwaambia ukweli watu wanaofanya mambo yasiyo na tija.

Nay wa Mitego

Wiki iliyopita msanii huyo alivunjiwa kioo cha gari lake na watu wasiojulikana wakati akienda kutambulisha video ya ya wimbo wake mpya wa 'Shika Adabu Yako' kwenye kipindi televisheni.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii rapa huyo, Nay ameweka picha ya gari hiyo ikiwa imevunjwa kioo huku akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kushindwa kuweka video hiyo kwa muda mwafaka kutokana na tatizo hilo.

Baada ya tukio hilo, msanii huyo aliiambia Nipashe kuwa hawezi kuvunjika moyo kutokana na kitendo hicho na anaamini ujumbe wa wimbo wake umewagusa walengwa.

"Mimi ninafarijika sana kwa sababu kile ambacho nimekikusudia kukifikisha kwa walengwa, kimefika na ninawaomba mashabiki wangu waendelee kuniunga mkono katika harakati hizi za kuelimisha watu kuachana na mambo yasiyofaa," alisema Nay.