wanaoshiriki onyesho la Coke Studio linalotarajiwa kuanza kuonyeshwa kwenye vituo vya luninga mapema Septemba mwaka huu.
Nahreel ambaye ameandaa nyimbo nyingi bora za wasanii mbalimbali nchini zinazotamba katika soko la muziki ndani na nje ya nchi, pia ni mmoja wa wanamuziki wa Kundi machachari la Nevy Kenzo.
Akizungumza kuhusu onyesho hilo jana akiwa Nairobi nchini Kenya, Nahreel alisema misimu minne ya Coke Studio Africa imekuwa na mafanikio makubwa katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava barani Afrika.
"Washiriki wamejiongezea mashabiki, wamejifunza mambo mengi kuhusu muziki kama burudani, muziki kama taaluma na muziki kama biashara na tena si tu kutoka kwa wasanii wenzao wa Afrika, bali wa Marekani pia," alisema.
Baadhi ya wakali wa kutengeneza muziki anaoshirikiana nao msimu huu ni Yuvir Pillay Nivedan a.k.a Sketchy Bongo kutoka Afrika ya Kusini na Kiff No beat kutoka nchini Ivory Coast.
Kwa upande wa Ma-DJ wapo Tafinha kutoka Angola, Laura Beg (Mauritius), Jah Prayzah na Slapdee (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Bisa Kdei na Worlasi (Ghana), Betty G (Ethiopia), Bruce Melodie, Shellsy Baronet na Mr. Bow (Msumbiji), Denise (Madagascar) na Freeda kutoka Namibia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Coca-Cola msimu wa Coke Studio mwaka huu utakuwa umesheheni burudani za muziki motomoto wenye vionjo vya Kiafrika kutokana na kuwaweka wasanii pamoja kutoka nchi 16 za Afrika na kushirikiana kufanya kolabo ambapo onyesho lake litaonyeshwa kwenye vituo vya luninga zaidi ya nchi 30 barani Afrika.
Wasanii wanaoshiriki Coke Studio msimu huu wanatokea katika nchi za Africa ya Kusini, Rwanda, Angola, Zimbabwe, Togo, Madagascar, Mauritius, Kenya, Uganda, Tanzania, Nigeria, Ghana, Msumbiji, DRC, Ethiopia na Cameroon.










