Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ulanga(CCM), Goodluck Mlinga.
“Tunayo sheria lakini ilikosa kanuni za kubana maudhui hasa upande wa mitandao, kwa sasa tumeshatunga kanuni na zimeanza kufanya kazi.
“Kuna baadhi ya wasanii walianza kufanya uhuni kwenye mitandao jana, tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond , amefikishwa polisi na anahojiwa kufuatia picha alizorusha,” alisema.
Alisema pia ameagiza Nandy naye apelekwe polisi na kuhojiwa na vile vile wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani huku pia akitoa wito kwa vijana kutoifanya mitandao ya jamii kuwa "kokoro" la kupeleka kila kitu na kuwakumbusha kwamba tamaduni lazima zilindwe.










