Kwenye droo hiyo iliyofanyika katika Tawi la NMB Mtwara, wateja 76 wa benki hiyo kiongozi na kinara wa fedha kidijitali nchini walishinda pesa taslimu na pikipiki moja zinazotolewa kila wiki. Akizungumza kabla ya zoezi la kuwapata washindi hao, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini,Janeth Shango, alisema wateja 75 watapata 100,000/- kila mmoja na mwingine kunyakua pikipiki aina ya Boxer wiki hii. Mbali ya droo za kila wiki ambazo mpaka sasa washindi 608 wameshinda zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 84 huku thamani ya zawadi za kila mwezi zilizonyakuliwa na washindi 102 ni kiasi cha Shilingi milioni 110, shindano hilo pia limehusisha droo mbili za kila mwezi ambapo washindi 98 wamenyakua Shilingi milioni 1 kila mmoja huku wanne wakishinda Boxer kila mmoja wao. Kwenye droo ya Ijumaa, mshindi wa Boxer wa raundi ya saba, Husna Baraka, ambaye ni askari polisi mkoani Mtwara, alikabidhiwa zawadi yake ya pikipiki.
Zimesalia siku 17 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.
Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote










