-hatua za kisheria.
Malima ametoa namba yake katika maadhimisho ya Kumbukizi ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika kimkoa katika Manispaa ya Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa mlezi wa CCM mkoa huo ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Mohamed Ally Kawaida amesema licha ya mkoa kuwa na viwanda vinne vya sukari ikiwemo cha Mtibwa, Kilombero I na II pamoja na kiwanda kipya cha mkulazi lakini kuna changamoto ya upungufu wa sukari nchini na kulazimika serikali kuagiza tani 100,000 kutoka nje.
Amesema tayari awamu ya kwanza ya shehena ya sukari kutoka nje imeshawasili huku serikali ikitoa bei elekezi ya kuuzwa kwa sh 2700 mpaka 3200 kulingana na maeneo na kwamba bei hiyo ni sheria hivyo wafanyabiashara wote wanapaswa kuuza kwa kuzingatia bei hizo.
“Nawakumbusha wafanyabiashara, Serikali tayari imetoa maelekezo mahususi kuwa sukari inauzwa mwisho sh 3200 kwa kilo na mwananchi akikuta anauziwa sh 3500 anipigie simu mimi mwenyewe kwa namba yangu 0784 612020 nitaenda mara moja kushughulika nao" amesema Malima
Mkuu wa mkoa huyo amesema upungufu uliojitokeza wa sukari nchini umechangiwa na viwanda kushindwa kuvuna miwa kutokana na mashamba yake kujaa maji kwasababu ya mvua za mafuriko na kusababisha uvunaji wa miwa kupelekwa viwandani kukwama..
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kawaida akizungumzia kuhusu suala la sukari,alisema Baraza kuu la umoja huo liliazimia kuhusu bei ya juu ya sukari inayoendelea kuuzwa hapa nchini na wafanyabiashara wakiwemo wa Morogoro na kutaka Serikali ilishughulikie suala hilo.
“Mkuu wa Mkoa uliposimama hapa umetoa namba yako ya simu kwa wananchi umekiri wewe kwamba unafahamu hata mimi ninazo taarifa kwamba hapa Morogoro wapo baadhi ya wafanyabiashara wanauza sukari kwa bei ya juu tofauti na iliyopangwa na Serikali” alisema Mwenyekiti huyo wa Taifa wa UVCCM.










