Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mathew Makwinya, alitoa agizo hilo alipokuwa akifunga kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani wiki iliyopita.
Makwinya alisema Halmashauri yao haina viwanda ambavyo vingesaidia kuongeza mapato yake, badala yake imekuwa ikitegemea malipo yatokanayo na ushuru wa mauzo ya mazao.
Aidha, alisema wananchi wanapaswa kuongeza juhudi katika kilimo cha korosho, ufuta, njugu na karanga; kwa kufanya kilimo cha kibiashara. “Mazao haya ndiyo yatakayosaidia kuinua mapato yetu, kutokana na ushuru utokanao na kuuza kwa mazao hayo,” alisema Makwinya.
“Chakula cha kupewa ni cha kupewa tu, hakilingani na kile ulicholima na kukivuna wewe mwenyewe,” alisisitiza.
Pia, aliwashauri madiwani kufanyakazi kwa ushirikiano bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuwapa ushirikiano watendaji wa Halmashauri yao.










