Wanahabari watakiwa kuielimisha jamii kuhusu chanjo

05Dec 2023
Neema Hussein
Rukwa
Nipashe
Wanahabari watakiwa kuielimisha jamii kuhusu chanjo

WAANDISHI wa habari kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe wametakiwa kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa chanjo hasa kwa watoto kwa lengo la kutokomeza magonjwa mbalimbali yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo surua na polio.

Wito huo umetolewa na Mkufunzi Danford Barnaba katika mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu habari za chanjo yaliyofanyika mkoani Rukwa.

Barnaba amesema waandishi wanaumuhimu mkubwa katika kuhakikisha wanaelimisha jamii iondokane na imani potofu kuhusu chanjo zinazotolewa kwaajili ya kuwalinda watoto na magonjwa kama polio, surua na saratani ya mlango wa kizazi.

Kwaupande wao waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wamesema watatumia elimu waliopata kuhakikisha wanaisaidia serikali kutokomeza magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari.