Kwa mujibu wa taarifa ya Ewura iliyotolewa inaeleza kushuka huko kunatokana na kupungua kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.
“Kwa mwezi Desemba, 2023 bei za mafuta (FOB) kwenye soko la dunia zimepungua kwa wastani wa asilimia 0.86 kwa mafuta ya petroli na asilimia 9.11 kwa mafuta ya dizeli. Aidha, gharama za kuagiza mafuta (premium) kwa Bandari ya Dar es Salaam, zimepungua kwa wastani asilimia 24 kwa mafuta ya petroli na asilimia 30 kwa mafuta ya dizeli,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Kwa Bandari ya Tanga gharama za kuagiza mafuta (premium) zimepungua kwa asilimia 30 kwa mafuta ya petroli na asilimia 17 kwa mafuta ya dizeli. Bartdari ya Mtwara haikupokea shehena ya mafuta."
Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Desemba 2023 kwa mujibu wa Ewura, yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 8.72; huku gharama za uagizaji wa mafuta zikishuka kwa kwa wastani wa asilimia 27 kwa petroli na asilimia 23 kwa dizeli.










