Wakutana kupeana mbinu usalama wa afya kazini

23Feb 2024
Halfani Chusi
Nipashe
Wakutana kupeana mbinu usalama wa afya kazini

KATIKA kuhakikisha masuala ya afya na usalama mahala pa kazi yanazingatiwa taasisi inayojihusiaha na Mambo ya Usalama Kazini Tanzania (TOHASA) imeandaa mkutano maalumu kwaajili masuala ya hayo.

Mkutano huo ambayo ni wa kwanza kufanyika nchini uliyofanyika Jana jinin Dar es Salaam uliwakutanisha wadau wa kampuni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Akizungumzia kwa niaba ya Serikali Katika Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka OSHA, Joshua Matiko amesema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa umewakutanisha na wataalam mbalimbali wa afya na usalama kazini.

 

Amesifu kitendo cha TOHASA, kuandaa mkutano huo akisistiza utaleta tija Katika utendaji wa kazi ndani na nje ya nchi.

 

Amesema serikali Katika nchi zote duniani zimejikita kwenye masuala ya usalama wa afya mahala pakazi na kwamba kila mtu anapaswa kulizingatia hilo.

 

Mwenyekiti wa TAHOSA, Coroline Balaza amesema mkutano huo utaleta mafanikio kwa kuwa umewakutanisha wataalamu na wafanyabiashara mbalimbali kubadilishana ujuzi na kutoka jawabu la pamoja Katika agenda hiyo.

 

Caroline amesema awali ilikuwa ni ngumu kukutana na wadau kujadili pamoja lakini kwa sasa imewezekana jambo alilosisitiza kwamba kwao ni mafanikio makubwa. 

 

"Ninashauri serikali iwatambue wataalamu wa usalama wa afya kazini sera zikiboresha na wataalamu wakihusishwa itasaidia kupiga hatua Katika eneo hilo" ameshauri Caroline 

 

Meneja wa Afya na Usalama Kazini Katika Mgodi wa Geita (GGML)Isaack Senya ambaye pia ni miongoni mwa walioshiriki mkutano huo amesisitiza kuwa ni muhimu kuzingatia afya za wafanyakazi.

 

Amesema mafuzo waliyoyapata pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka kampuni nyingine yatawasaisia kuboresha zaidi masuala ya afya kazini kwao. 

 

Ametamba kuwa kwa sasa wana zaidi ya miaka 10 bila mfanyakazi kupoteza maisha akiwa kazini na kwamba semina hiyo itawafanya kupata mafanikio makubwa zaidi kwenye eneo hilo.

 

"Ninashauri kampuni nyingine kushiriki kama hizi ili kujua namna ya kulinda afya na usalama wa mfanyakazi mahali popote. Mfanyakazi anapoumia au kupoteza maisha akiwa kazini ni hasara kubwa kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye kampuni. 

 

"Wale ambao hawajapata hii fursa, wajue kulinda afya ya mfanyakazi ni takwa la kisheria ni wajibu kuhakikisha wafanyakazi wanabaki na afya nzuri za kuweza kuhudumia familia zao" amesema 

 

David Ongesa Rais wa Usalama Mahala pa kazi Kenya (WSPAK), ambaye pia ni miongoni mwa washiriki alisema ni fahari kushiriki semina hiyo akiwa Tanzania kwa kuwa itamuongeza ujuzi na kwenda kusaidia kubor

esha nchini kwako.