Akipokea msaada huo, Janeth amesema msaada uliotolewa na Tigo umegusa waathirika kwa kiasi kikubwa sana hasa kwa kuzingatia mahitaji yao.
"Ni msaada wenye thamani kubwa kwa wenzetu hawa, umegusa mahitaji yao muhimu, magodoro yaliyotolewa moja kwa mona yanaenda kutatua suala la malazi," amesema Janeth.
Aidha ameziimiza kampuni na taasisi nyingine kuiga mfano wa Tigo, kuja kujitolea kwa chochote watakachojaaliwa.Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya ameeleza namna walivyoguswa na tukio hilo na ndio sababu ya kufikia maamuzi ya kutoa msaada kusaidia waathirika hao.
" Ili janga ni la watanzania wote, kila mmoja naamini ameguswa na tukio hili, Tigo tunaungana na watanzania wengine kuwapa pole waathirika wote na msaada huu unaweza kusaidia kwa wenzetu hawa," amesema Mainoya.










