Maafisa hao wa TFDA wa Kanda ya Kaskazini walifanikiwa kufika katika kiwanda baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kufanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali zenye uzito wa zaidi ya tani saba.
Akizungumza katika tukio hilo, afisa wa TFDA Kanda ya Kaskazini, Benson Cheza, alisema mmiliki wa kiwanda hicho amekuwa akileta maombi ya muda mrefu ya kutengeneza vipodozi hivyo lakini alikuwa hajapewa majibu kama aanze kutengeneza.
Aidha alifafanua kuwa mmiliki huyo amefanya utangenezaji kabla ya kuruhusiwa hivyo wao kama TFDA hawatosita kumchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuteketeza bidhaa hizo kwa garama zake.
Mmiliki huyo, Makala Chalo alikiri kutengeneza bishaa hizo lakini akasema zina uhalali kutokana na kuwa na vibali vya utengenezaji wake.
Aliema ameruhusiwa na mamlaka husika na kupewa kibali cha kutengeneza bidhaa hizo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kata ya Kiranyi Jane Sirikwa alisema wao kama serikali ya kata hawakuwa na taarifa na utengenezaji wa bidhaa. Aliwataka wananchi kuwa makini na utumiaji wa vipodozi ambavyo havijathibitishwa chakula na dawa.










