Ndaki alitoa rai hiyo katika mahafali ya 47 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka wilayani hapa. Alisema wazazi wanatakiwa kuangalia fursa za kusoma kwenye vyuo vya ufundi ili waweze kujiajiri badala ya kusubira ajira serikalini ambazo kwa sasa hakuna.
“Nitatoa mfano mzuri kwa watoto wangu licha ya kumaliza vyuo vikuu hakuna aliyeajiriwa mbali na mimi kuwa na uwezo wa kuongea uso kwa uso na waziri mwenye dhamana. Wazazi somesheni watoto mkijua ajira kwa sasa hakuna serikalini changamkieni fursa za ufundi wajiajiri,” alisema Ndaki.
Mhitimu wa chuo hicho, Josephina Lucas, alisema kati ya wanafunzi walioanza masomo ya ufundi chuoni hapo 135 ni 124 wamehitimu.
Rais wa Wanafunzi wa chuo hicho, Charles Joseph, alisema elimu aliyopata na wahitimu wenzake, itawasaidia kuingia moja kwa moja kwenye soko la ajira kwa kujiajiri wenyewe.
Akitoa taarifa ya chuo hicho, Mwalimu Noel Shigolo, alisema kilianza kutoa mafunzo mwaka 1978 kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata elimu ili kuondokana na adui umaskini, ujinga na maradhi.
Mkuu wa chuo hicho, Michael Mahundi, alisema serikali imetoa mashine za kisasa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vyenye thamani ya Sh. milioni 208 za Covid 19.
Mahundi, alisema serikali imetoa zaidi ya Shilingi milioni 300 kwa ukarabati, ujenzi wa jengo la utawala, madarasa, vyoo na mabweni.
Kwa upande wake, Rais wa wanafunzi wa chuo hicho, Charles Joseph, alisema elimu aliyopata na wahitimu wenzake, itawasaidia kuingia moja kwa moja kwenye soko la ajira kwa kujiajiri wenyewe.










