Halotel inalenga kuwa chachu kuboresha Uchumi wa Kidigitali Tanzania

29Nov 2023
Zuwena Shame
Nipashe
Halotel inalenga kuwa chachu kuboresha Uchumi wa Kidigitali Tanzania

Kampuni ya  Halotel Tanzania imeazimia kuwa chachu katika enzi ya kidigitali, ikiongoza katika suluhisho na huduma za ubunifu zinazokidhi mahitaji ya kimawasiliano yaliyojikita katika kuboresha na kuunganisha jamii kidigitali.

Halotel Tanzania imekuwa ikitoa huduma na suluhisho za ubunifu kwa watanzania na jinsi wanavyounganisha na kusimamia maisha yao ya kila siku.

Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Tanzania, Abdallah Salum alisema kuwa katika mazingira ya kidigitali yanayobadilika haraka kipindi hiki, mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na hivyo Halotel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa suluhisho za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa wateja wa kampuni hasa katika sekta ya benki, mashirika yasiyo ya kiserikali, na kadhalika.

Salumu, alisema kuwa katika kutambua jukumu muhimu la teknolojia katika tasnia ya biashara ya kisasa, Halotel imejumuisha kikamilifu suluhisho za Tehama ili kuboresha ufanisi wa uendeshaji, usalama, na uzoefu kwa wateja wake. 

"Azma ya kampuni ya kufanikisha mabadiliko ya kidigitali inaonekana katika suluhisho zake maalum za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, zikihakikisha kuwa benki na biashara zinaweza kufanikiwa katika mazingira yanayozidi kuwa ya kidigitali."alisema Salum.

Aliongeza kuwa mafanikio ya kuvutia ya Halotel ni kutokana na kutoa huduma za mawasiliano za daraja la kwanza kwa zaidi ya vijiji 18,720, kuweka zaidi ya kilomita 18,000 za miundombinu ya fibre.

"Kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, tumefikia vijiji zaidi ya 1,002, hivyo kufanya idadi ya vijiji ambavyo Halotel imeviunganisha na mawasiliano kufikia zaidi ya 20,700, na hivyo kuendelea kukuza dhamira yetu ya kuwa mtandao wa kwanza ulioenea maeneo mengi nchini hasa vijijini. Hii inathibitisha dhamira yetu kwa Ajenda ya Uunganishaji Inayojali, kuhakikisha hata watanzania walioko mbali wanapata huduma za mtandao na mawasiliano". alisema Salumu.

Aidha Salum aliongeza kuwa Kwa kutoa huduma kwa gharama nafuu na za kuaminika, Halotel haiunganishi watu tu bali inaondoa daraja katika upatikanaji wa huuma za kidigitali kwa jamii ya watanzania na kuboresha zaidi utumiaji wa huduma za mawasiliano wakisasa wa kidigitali.

Aliitaja MyHalo ambayo ni moja ya ushahidi wa dhamira ya Halotel kuwarahisishia wateja utumiaji wa mawasiliano inayoweza kutumika kirahisi huwapa fursa watumiaji kupata huduma zote za Mawasiliano ya Halotel kwa urahisi.

" Application hii ni nzuri kwani inarahisiha mawasiliano kutoka kupigia simu marafiki na watu mbalimbali, hadi kuangalia salio la akaunti, na hata kununua data au muda wa maongezi. Application ya MyHalo imekuwa huduma ya muhimu kwa wateja wa Halotel kwa wao kupata huduma zote kiganjani, popote walipo." aliongeza. 

Alisema kuwa Halotel pia imekuwa na jukumu muhimu katika ujumuishaji wa kifedha kwa kuanzisha HaloPesa, Kupitia App ya HaloPesa na huduma za E-wallet, Halotel imewawezesha wateja wake kufanya miamala salama na rahisi ya kifedha, kuanzia uhamisho wa fedha na malipo ya bili mbalimbali, hadi kufanya manunuzi na kupata huduma mbalimbali za kifedha, zote kutoka kwenye kiganja cha mikono yao.

"Usalama na upatikanaji rahisi wa huduma zetu za kifedha unampa demokrasia mamilioni ya wateja katika miamala ya kifedha. Suluhu zetu zinachangia ujumuishaji wa kifedha na kuweka msingi wa uchumi usiohitaji kutembea na pesa, na kuwezesha watu binafsi kushiriki kikamilifu katika mfumo wa ikolojia wa kidijitali” alisema Salum.

 Alisema kuwa huduma ya Haloyako pia inawawezesha wateja kufikia malengo yao ya kifedha na kuboresha maisha yao ya kila siku ambapo mteja anathaminiwa na kile au kidogo alicho nacho ili kufanya akiba kwa ajili ya siku zijazo.

"Huduma hii yenye ubunifu hutoa mwendelezo na uhuru kwa watumiaji, ikisaidia kuendeleza utamaduni wa kuweka akiba na nidhamu ya kifedha. Haloyako ni zaidi ya huduma ; ni dhamira thabiti ya kusaidia watu binafsi kufikia matarajio yao ya kifedha. Huduma hii inaleta pamoja watu wa ngazi zote na hivyo kuishi kaulimbiu ya "Pamoja kwa Ubora," aliongeza Salum.