-katika nafasi hiyo mwaka 1980.
Natepe alimrithi Rais mstaafu Mwinyi kwenye wizara hiyo na baadaye aliteuliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na Nipashe, msemaji wa familia ya marehemu Natepe, Ismail Said alisema kwamba wamesikitishwa na taarifa hizo ambazo familia haifahamu nia yake ni nini, akisema kwamba ni za kupotosha hutoka kila inapokaribia uchaguzi mkuu.
“Baba yetu alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wakati Hayati Julius Nyerere akiwa Rais. Tumezaliwa na kukulia Upanga jijini Dar es Salaam tangu mwaka 1977. Mpaka sasa tunaishi Upanga na hatujawahi kuishi Oysterbay ambako kuna hiyo nyumba ambayo Mwinyi aliishi.”
Alisema taarifa hizo zinachapishwa ili kuharibu taswira ya familia na kuwaonya wote walionyuma ya taarifa hizo na kuzisambaza kuacha kabla sheria haijachukua mkoando wake.
Alisema kwa sasa familia inafanya kazi na vyombo vya dola ikiwamo Jeshi la Polisi kuwasaka watu wanaosambaza taarifa hizo ambazo zinaleta chuki kati ya watu na watu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais mstaafu Mwinyi alihudumu kama waziri katika wizara hiyo mwaka 1975 hadi 1976 wakati Natepe (marehemu) alihudumu kuanzia mwaka 1980 hadi 1983.
Kadhalika katika kitabu chake cha safari ya maisha yangu, Rais Mwinyi ameandika kwamba aliishi Oysterbay kabla ya kufanyika kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri mwaka 1976 na alihamishiwa kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kwenye kitabu hicho, Rais mstaafu Mwinyi anasema baadaye alihamishiwa kwenda wizara inayoshughulikia Muungano, hatua hiyo ilimlazimu ahamie Zanzibar kwa sababu makao makuu ya wizara yalikuwa huko na kuiacha nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Oysterbay waziri mpya aliyechukua nafasi yake, kwa wakati huo alikuwa ni Jackson Makweta.










