Wanafunzi Soweto walivyojitoa mhanga kuwakabili makaburu

21Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wanafunzi Soweto walivyojitoa mhanga kuwakabili makaburu
  • *Polisi wana silaha nzito, wao wana mawe

ALFAJIRI ya Juni 16, 1976, maelfu ya wanafunzi kutoka mji wa waafrika wa Soweto, nje kidogo ya Johannesburg, walikusanyika kwenye shule zao kwa lengo la kushiriki katika tukio lililoandaliwa na wanafunzi ili kupinga udhalilishaji.

Wengi wao walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na ujumbe uliosomeka 'Down with Afrikaans' na ‘Elimu kwa Wabantu’ iende kuzimu’ .

Baadhi yao, walikuwa wanaimba nyimbo za uhuru.Mkusanyiko huo wa wanafunzi haukuwa na silaha zozote. Walikuwa wanatembea kuelekea kwenye uwanja wa mpira wa miguu ujulikanao Orlando soccer stadium yalikopangwa kufanyika maandamano ya amani

Tukio hilo, lilikusanya wanafunzi zaidi ya 10,000 kuelekea kwenye uwanja huo. Askari polisi wapatao hamsini hivi walijaribu kuwasimamisha wanafunzi hao na kuwataka wageuze kurudi nyuma walikotoka.

Mwanzoni askari hao walijaribu bila ya mafanikio kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi huku wakionyesha alama za kuwatahadharisha

Baadaye polisi walifyatua risasi za moto kwenye mkusanyiko huo uliokuwa ukiandamana.Wanafunzi wengi walijibu kwa kukimbilia kuelekea kwenye kambi zao huku baadhi yao walijaribu kukabiliana na polisi kwa kuwarushia mawe.

Siku hiyo ,wanafunzi wawili , Hastings Ndlovu na Hector Pieterson, walikufa kutokana na kupigwa risasi na polisi ,mamia walijeruhiwa katika mkanganyiko huo uliotekelezwa Soweto.

Mashambulizi hayo ya Soweto yalisababisha taarifa zisambae kwa kasi kubwa na kufika kwenye maeneo zaidi ya 100 ya mijini na vijijini nchini kote Afrika ya Kusini.

Kilichosababisha hasa maandamano hayo ya Juni 16, 1976, ni wanafunzi kupinga sheria iliyotolewa na Idara ya Elimu ya Bantu (The Bantu Education Department) ambayo ilitaka lugha ya Afrikaans itumike kama lugha rasmi kufundisha nusu ya masomo katika shule za kati (middle school ) na za sekondari (High school)

Tangu wanachama wa chama tawala (National Party) walipozungumzia Afrikaans, wanafunzi weusi waliitafsiri kuwa ni lugha ya ukandamizaji. Zaidi ya hapo, walimu waafrika na wanafunzi wakaanza kupata uzoefu hasi kuhusu sera ya lugha hiyo darasani.

Mlipuko huo wa Soweto uliibuka baada ya muongo mmoja wa vuguvugu la kianaharakati la kupinga mwenendo usiofaa toka serikali ya kibaguzi kuanzia miaka ya 1960.

Hivyo katika kipindi cha ‘muongo mmoja wa ukimya’ kumbe vuguguvu la upinzani likawa linachemka
Mwaka 1969, wanafunzi weusi wakiongozwa na Steve Biko (miongoni mwa wengine), walianzisha Chama cha Wanafunzi wa Afrika (the South African Student's Organization -SASO). Walipania kubainisha kujivunia uafrika wao, kujitegemea, na ukombozi wa kisaikolojia , Mwamko wa harakati za mtu mweusi mnamo mwaka 1970 ukawa na nguvu za ushawishi katika miji mingi ikiwamo Soweto.

Vuguvugu la kisiasa la mwaka 1976 lilichochewa na kuibuka kwa athari za migomo ya huko Durban mwaka 1973; ukombozi wa nchi jirani ya Angola na Msumbiji mwaka 1975; na ongezeko la usajiri wa wachezaji katika shule za watu weusi, zilichangia kuanzishwa kwa hali ya dharura ya vitambulisho vipya kwa vijana.

Licha ya kuwa wanafunzi watoto wanaweza kuwa wameshawishiwa na Mwamko wa Harakati za Watu weusi ( the Black Consciousness Movement mwaka 1970, wanafunzi wengi wa zamani wa Soweto hawakumbuki kuhusishwa kwa ushawishi mwingine kutoka nje ya taasisi yao au harakati za ukombozi katika maamuzi yao ya kupinga matumizi ya lugha ya Afrikaans katika shule zao.

Katika kumbukumbu yake , Sifiso Ndlovu, mwanafunzi wa zamani wa shule iitwayo Phefeni Junior Secondary School ya Soweto, anakumbukia namna gani Januari mwaka 1976 yeye na wanafunzi wenzake walivyokuwa na mtazamo wa kufanya vizuri masomo yao lakini namna gani matumizi ya lugha ya Afrikaans yalivyoshusha uwezo wa kufikia malengo yao (Hirson 175-77; Brooks and Brickhill 46) Echoing Ndlovu, ambaye sasa ni mbunge anakumbuka "Ilikuwa ngumu sana kubadilisha kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Afrikaans katika muda huo."

Kufukuzwa kwa walimu huko Soweto ambao walishindwa kutekeleza sera ya matumizi ya lugha ya Afrikaans kulichangia mkanganyiko mkubwa miongoni mwa wanafunzi wa madarasa ya shule za kati, ambao baadaye walianzisha maandamo madogo na kupinga kuingia darasani mapema miezi ya Mach, April na Mei .

Inakadiriwa kuwa wanafunzi wapatao 20,000 walishiriki katika upinzani huo . Walikumbana na hasira za polisi zisizo na chembe ya huruma hata chembe.

Idadi ya waandamanaji waliouawa na polisi inadaiwa kuwa ni 176, lakini makadirio yanafikia hadi 700 hivi Kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo, Juni 16 ya kila mwaka sasa ni sikukuu ya umma nchini Afrika Kusini ijulikanayo, Siku ya Vijana

Sababu ya upinzani

Wanafunzi weusi wa Shule za kati za Afrika Kusini huko Soweto walipinga sheria ya kutaka lugha ya Afrikaans ya mwaka 1974, inayowalazimisha shule zote za waafrika weusi zitumie lugha ya Afrikaans na Kiingereza kwa uwiano wa 50–50 kama lugha za kufundishia

Mkurugenzi wa Kanda wa Elimu ya Wabantu (Mkoa wa Kaskazini ya Transvaal), J.G. Erasmus, aliwaambia wakaguzi na Wakuu wa Shule kwamba kuanzia Januari 1, 1975, lugha ya Afrikaans itumike kwa masomo ya hesabu na masomo ya sanaa kuanzia darasa la tano (7th grade), kwa mujibu wa sheria ya Afrikaans ; kwamba lugha ya Kiingereza itakuwa ya kufundishia kwa masomo ya sayansi na mafunzo kwa vitendo (maarifa ya nyumbani, ushonaji, useremala, uhunzi, sanaa, sayansi ya kilimo)

Lugha za wenyeji zitatumika kwa ajili ya masomo ya dini,muziki, na utamaduni
Chama cha Afrikaans ambayo ilichukuliwa ni lugha ya kibaguzi iliwataka waafrika weusi kupendelea kiingereza.

Hata Bantustan nao walichagua Kiingereza na lugha za kienyeji za waafrika kama lugha rasmi ya waafrika
Kwa kuongezea , lugha ya Kiingereza ilikuwa inapata umaarufu wa kutumika katika mawasiliano ya biashara na viwanda .Sheria ya mwaka 1974 ililenga kulazimisha lugha hiyo miongoni mwa Waafrika weusi.

Wakati shule zote zilikuwa zinatumia lugha zote mbili za Afrikaans na Kiingereza , wanafunzi wazungu walikuwa wanasoma masomo mengine kwa lugha zao za nyumbani.

Punt Janson, aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu ya Bantu kwa wakati huo, alikaririwa akisema kuwa " Watu weusi wanaweza kufundishwa kufanya kazi shambani au kiwandani. Wanaweza kufanya kazi kwa mwajiri anayeweza kuwa anamudu kuzungumza lugha ya Kiingereza au Afrikaans-na mtu anayepaswa kumpa maelekezo anaweza kuwa anamudu kuzungumza kiingereza au Afrikaans.

“ Kwa nini sasa tukwaruzane kuhusu lugha ya kufundishia miongoni mwa watu weusi? Hapana sikufanya majadiliano nao na sitafanya majadiliano nao. Nimefanya majadiliano na Katiba ya Jamhuri ya Afrika Kusini …"

Sheria hiyo ilitungwa maalum ikiwalenga watu weusi, kwa sababu Afrikaans kama ilivyotafsiriwa kwa maneno ya Desmond Tutu, askofu wa Lesotho na msimamizi wa Johannesburg—kwamba "ni lugha ya wakandamizaji".

Vyama vya walimu kama vile Chama cha walimu waafrika wa Afrika Kusini, waliipinga sheria hiyo
Mabadiliko ya lugha ya kufundisha yaliwalazimisha wanafunzi kutilia mkazo wa kuijua lugha badala ya kuelewa masomo husika. Hii ilisababisha ufanyike uchambuzi na kuzuia uchambuzi wa kufikiri kwa kina.

Vuguvugu hilo liliendelea kukua hadi April 30, 1976, watoto wa shule iitwayo Orlando West huko Soweto walipogoma, wakipinga kwenda shule. Msimamo wao kisha ukasambaa katika shule nyingine za Soweto.

Wanafunzi weusi wa Afrika Kusini walipinga kwa sababu waliamini kuwa, wanastahili kutendewa na kufundishwa sawa na wanafunzi weupe wa Afrika Kusini. Mwanafunzi kutoka shule iitwayo Morris Isaacson, Teboho "Tsietsi" Mashinini, alipendekeza mkutano ufanyike Juni 13, 1976 ili kujadili nini cha kufanya.

Wanafunzi walianzisha Kamati maalum ya kushughulikia suala hilo baadaye ikajulikana ( the Soweto Students' Representative Council),ambayo iliandaa maandamano ya Juni 16, ili kuwafanya wasikike.

Hector Pieterson alibebwa na Mbuyisa Makhubo baada ya kupigwa risasi na polisi wa Afrika Kusini. Dada yake, Antoinette Sithole, alikimbia akifuatilia kando yao.

Pieterson baadaye alikimbizwa katika kliniki ya jirani na kutangazwa kuwa amekufa mara tu baada ya kufikishwa kituoni hapo.

Katika maandamano hayo inakadiriwa kuwa wanafunzi kati ya 10,000 na 20,000 walishiriki. Vuguvugu la upinzani huo lililoandaliwa na Soweto Students' Representative Council's (SSRC) kwa kuungwa mkono na Kikundi cha wanaharakati Weusi na walimu wa Soweto pia waliunga mkono maandamano hayo baada ya Kamati maalum kuelezea kuhusu hatua za kinidhani na amani zitakazochukuliwa.

Tsietsi Mashinini aliwaongoza wanafunzi kutoka shule ya Morris Isaacson ili kujumuika na wengineo, walitembea kutoka shule ya Naledi .Wanafunzi walianza kutembea na kujikuta polisi wakiwasubiri na kuweka bango barabarani lililowakataza kufanya hivyo katika barabara waliyopanga.

Viongozi wao wa kamati maalum waliutaka umma huo wasiwakabili polisi, hivyo maandamano yaendelee katika barabara nyingine ambayo hatimaye ikaishia jirani ya shule ya Orlando

Waandamanaji wanafunzi kati ya 3,000 na 10,000 walielekea katika eneo jirani ya shule. Wanafunzi walikuwa wanaimba huku wakionyesha mabango yaliyoandikwa kama vile, "Afrikaans izikwe ", "Viva Azania" na "kama sisi tutatumia Afrikaans, Vorster naye lazima atumie lugha ya Zulu".

Polisi waliwafungulia mbwa wakawaelekeza kwa waandamanaji ambao walijibu mapigo kwa kuwaua.Polisi wakaanza kuwafyatulia risasi wanafunzi.

Mmoja wa wanafunzi waliopigwa risasi na kufa alikuwa na umri wa miaka 13 Hector Pieterson. Alipigwa risasi katika shule ya Orlando West ambaye akachomoza kama alama ya mapambano ya Soweto

Polisi waliendelea kuwashambulia waandamanaji na watu 23 walikufa katika siku ya kwanza ya Soweto. Miongoni mwao alikuwa ni Dk Melville Edelstein, ambaye alikuwa ameyatoa maisha yake kwa ajili ya kazi za kijamii miongoni mwa watu weusi. Alishambuliwa kwa mawe hadi kufa na umma huo kisha kuachwa shingoni akiwa na bango lililosomeka "Jihadhari na Afrikaners"

Vurugu zilishika kasi hadi kwenye baa na maduka ya kuuza bia—ambayo yalichukuliwa kama ni sehemu zinazounga mkono serikali ya ubaguzi—yalilengwa. Magari ya polisi na yale yaliyobeba silaha za kivita yakawa yanarandaranda mitaani hadi usiku kucha.

Kliniki zikawa zinachukua hatua ya dharura ya kupokea majeruhi hata kuzidiwa na idadi kubwa ya watoto waliokua wanavuja damu. Polisi ikawataka kutoa orodha yote ya wale waliofikishwa hapo wakiwa na majeraha ya risasi. Viongozi wa hospitali walipeleka taarifa hizo kwa madaktari waliokataa kuandaa orodha hiyo.

Polisi wapatao 1,500 wakiwa na silaha nzito walipelekwa Soweto Juni 17 wakiwa wameba silaha nzito mbalimbali walirandaranda wakiwa ndani ya magari ya deraya huku helkopta zikipita juu kukagua hali ilivyo. Jeshi la Afrika Kusini pia lilipewa amri ya kukaa tayari.

Idadi ya watu waliokufa ni 176 na wanakadiriwa kufikia 700. Idadi ya kwanza ya serikali iliwataja wanafunzi 23 tu waliouawa na waliojeruhiwa walikadiriwa kufikia zaidi ya elfu moja.