Maandalizi ya maashindano hayo yanayotarajia kushirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka nchi zote za zote za ukanda huo, tayari yameanza chini ya chini ya usimamizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Kaimu katibu mkuu wa shirikisho hilo, Omben Zavalla, aliiambia Nipashe jana kuwa nchi 11 (zikiwamo tano za A. Mashariki) zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo.
Alizitaja baadhi ya nchi ambazo tayari zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo kuwa ni mwenyeji Tanzania, Zanzibar (itashiriki kama nchi), Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan, Elitrea na Ethiopia.
"Nchi nyingi ambazo tumezitumia mwaliko, zimerejesha majibu ya kuthibitisha ushiriki wao," alisema Zavalla huku akiomba wadhamini wajitokeza kusaidia mashindano hayo.
Alifafanua kuwa mbio hizo zitakuwa za kilomita 100, hadi 3,000 kwa wanariadha vijana kutoka nchi hizo.
Aidha, kiongozi huyo alisema kuwa kabla ya mashindano hayo, kutakuwa na mkutano mkuu wa viongozi wa nchi hizo ukiwa na lengo la kuzungumzia mambo mbalimbali yahusuyo mchezo huo.
Katika hatua nyingine, RT imewataka wanariadha wa timu ya taifa ya Tanzania kutumia muda ulioongezwa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kufuzu michezo ya Olimpiki
Tanzania mwenyeji riadha A. Mashariki
04Feb 2016
Nipashe
Tanzania mwenyeji riadha A. Mashariki
TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana ya riadha ya Afrika Mashariki yaliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari 22-23.










