Dar es Salaam ni wenye historia ndefu. Uliwahi kuitwa majina ya Mzizima na Bandari ya Salama. Ulijulikana kwamba ni mji mkubwa nchini, unaopatikana pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
Dar es Salaam pia ulitambulika kama mji muhimu wa kibiashara na msamiati ‘Mzizima’ ulimaanisha mji wenye neema. Chimbuko la mji huo unaanzia mwaka 1857.
Historia ya Mzizima ilianza tangu miaka 1000 iliyopita, kwa watu wa Bara waliojichanganya na Wazaramo, walitulia na kulima katika maeneo ya maji Magogoni (kwa sasa kivukoni), Mjimwema na Gezaulole.
Mji wa Dar es Salaam ulianza kuonyesha mabadiliko kutokana na ujio wa Masultani, Wajerumani na Waingereza.
Mwaka 1866, Sultan Seyyed Majid wa Zanzibar, aliupa jina la ambalo ndilo linalotumika sasa neno la kiarabu lililomaanisha ‘Mbingu ya Amani.’
Baada ya kifo cha Sultan Majid mwaka 1870, Dar es Salaam ilianguka, lakini iliinuka tena mara baada ya ujio wa kampuni ya Kijerumani -German East Africa Company, iliyoanzisha kituo cha biashara mwaka 1887 na kuuondoa utawala wa Kiarabu, hata kutawala Pwani ya Afrika Mashariki.
Walianzisha mamlaka ya kusimamia mambo mbalimbali ndani ya Afrika Mashariki na biashara, kwa ajili ya maendeleo ya reli ya kati.
Iliweza kukua kwa haraka kutokana na utawala, pamoja na biashara ya Wajerumani katika Afrika ya Masahriki. Mwaka 1891 ilifanywa kuwa Mji mkuu wa kampuni ya German East Africa.
Wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia, utawala wa Kijerumani uliangushwa na Waingereza na tangu hapo taifa ilijulikana kama Tanganyika.
Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Dar es Salaam ilikuwa haraka katika zama hizo ambazo kulianzishwa kwa chama cha TANU iliyoipatia uhuru, mwezi Desemba 1961.
Dar es Salaam iliendelea kuwa mji mkuu mpaka ulipohamishiwa Dodoma mwaka 1973. Ulipo mkoa huo ni katikati ya nchi cha Tanzania. Licha ya kuwa a kuwa makao makuu ya serikali historia ya Ujerumani, imekuwa ikionekana jiji katikakti ya Dar es Salaam ni mji muhimu kwa biashara na serikali.
MAKONDA KUFUFUA BIASHARA
Mkuu wa Mkoa Makonda anasema kuwa wakati historia iki Jiji la Dar es Salaam kitovu chake ni biashara, inamsukuma afufue kwa vitendo.
Makonda anasema, anaanza kwa kufunga taa katika maeneo yote ya jiji, ili kufufua taswira yake na kuondokana na utaratibu wa wafanyabishara kufunga biashara zao mapema.
Anasema taa hizo zitatumiwa na wafanyabishara kufanya biashara hadi usiku wa manane.
“Ni aibu tunauita mji huu kuwa wa kibiashara lakini usiku maduka yote yanakuwa yamefungwa. Taswira ya mji wa Dar es Salaam ni biashara kufanyika wakati wote na hata wanaotoka nje ya mji wa nje ya nchi kupata bidhaa wanazozihitaji kwa wakati,” anasema.
Akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) katika mkutano wao wa mwaka uliojumuisha wafanyabiashara zaidi 300 kutoka mikoa yote nchini nchini, Makonda anasema wakati wa jiji la Dar es Salaam kuwa jiji la biashara umewadia.
“Ni jambo la aibu wafanyabishara wa Kariakoo wanashindwa kufanya biashara zao hadi usiku na kufunga jioni wakati kuna watu wanatoka kazini usiku na wanataka kununua bidhaa lakini wanazikosa,” anasema.
Anasema kabla ya kuanza kutekeleza dhana hiyo, alianza kwa kukaa na baadhi ya wafanyabishara ili kubaini changamoto zinazowakabili na kushindwa kuboresha biashara zao hadi usiku.
Kwa mujibu wa Makonda, baada ya kukaa na wafanyabishara hao walimueleza sababu za kutofanyabiashara hadi, sababu kuu ni ulinzi duni.
Wafanyabisahara walimueleza namna wanavyokosa mwanga wa kutosha, kuendelea na biashara zao na hivyo wanalazimika kufunga mapema.
Anasema changamoto nyingine waliyomueleza, ni kukithiri vibaka na wezi wanaoendesha wizi katika meaneo hayo ya biashara.
Mara baada ya kupokea changamoto hizo, Makonda anasema alianza kuangalia namna jiji linavyokuwa giza kwa kukosa taa katika barabara zote.
“Juzi usiku nilifanya ziara ya kukagua taa za barabarani, jambo la kushangaza nilikuta sehemu kubwa ya mji ukiwa ni giza. Hivyo tumeshaanza kutekeleza ufungaji wa taa katika maeneo yote ili kulipendezesha,” anasema.
Kwa mujibu wa Makonda, baada ya ukaguzi hatua inayuata hatua iliyofuata aliwaagiza wakurugenzi kuanza kufunga taa katika maeneo yote ya barabara ili kuufanya mji kuwa mweupe.
Anasema baada ya hatua hiyo, kitakachofuata ni kuangalia namna wafanyabiashara wanaweza kufanyabishara zao hadi usiku.
Makonda anasema changamoto ya vibaka anaifanyia kazi na kwamba katika mkoa huo, jumla Polisi zaidi ya 300 ambao wameanza kujipanga ili kukabiliana na uhalifu huo.
Anasema jambo la kwanza ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zake pamoja na kuondoka na uhalifu katika maeneo ya biashara.
JENGO L MACHINGA
Wakati Makonda anajipanga kuboresha mfumo wa kibiashara jijinii. pIa anakabidhiwa jengo la Machinga Complex lililojengwa na Halmashauri ya jiji la Sa res Salam, kwa ajili ya kuwezesha wafanyabishara wadogo maarufu kama Machinga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene ndiye aliyemkabidhi jengo hilo ili alisimamie na kuhakikisha wafanyabishara wadogo ndio wanaofanyabiashara ndani ya jengo hilo.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kubainika kuwa, wafanyabishara walioko kwenye jengo hilo ni wanasiasa na watendaji wa serikali waliohodhi vizimba na kuvipangisha kwa wajasiriamali badala ya wamachinga ambao ndio walengwa.
Simbachawene alimuagiza Makonda, kuanza kulisimamia rasmi, baada ya kutangaza kuifuta bodi iliyokuwa ikiliendesha pamoja na kumfuta kazi meneja wa soko hilo na watumishi wote.
Makonda, aliagizwa kuwapa jengo hilo wafanyabishara wadogo ambao ni machinga wa eneo hilo pamoja na wale wa Karume.
Akipokea maelekezo hayo, Makonda anaahidi kutekeleza agizo hilo na kusimamia vyema sekta hiyo ya biashara kwa jiji la Dar es Salaam.
Changamoto za Wafanyabishara
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Johnson Minja, anabainisha changamoto zinazowakabili wafanyabishara ni kukosa maeneo rasmi ya kufanyia biashara.
“Serikali itenge maeneo kati ya makazi na maeneo ya biashara pamoja na biashara kutofautishwa katika maeneo,” anasema.
Anasema changamoto nyingine, ni serikali kutoshirikiana kutatua malalamiko yao.
Minja anasema pia kilio chao ni bei elekezi kwa biashara zinazoshushwa bandarini, ili kuondoa urasimu kwa walanguzi wa kodi unaofanywa na watumishi wasiyo waaminifu.
“Kama kodi tukilipa halali kule bandarini ni wazi kuwa suala la kutumia mashine za EFDs halitakuwa jambo gumu na kila mmoja atatekeleza agizo hilo, kwani kinachosumbua ni serikali kuacha kutumia bei elekezi kutolea mizigo bandarini,” anasema Minja.
Anasema changamoto nyingine ni sekta hiyo kutopewa kipaumbele na serikali pamoja na wafanyabishara kudhalilishwa na wakusanya kodi ambao mara ngingine hutumia mgambo wa jiji.
Minja anasema serikali ikisimamia vyema sekta hiyo ni wazi itaongoza kwa uchumi wa Taifa kwani kizazi hiki, kilimo kimekuwa siyo tena uti wa mgondo bali biashara.










