Stephe Jacob 'JB' ni msanii mkongwe wa filamu nchini ambaye anaamini kwamba wasanii wa fani hiyo kwa sasa wanatakiwa kuboresha kazi zao kwa kutumia kampuni za hapa nchini badala ya kukimbilia nje.
Msanii huyo aliiambia Nipashe kuwa kwa muda mrefu baadhi ya wasanii wamekuwa wakiandaa filamu na kufuata wenzao wa nje na kuwashirikisha kwa lengo la kupata ubora.
"Ninaamini kwamba filamu kubwa na bora zitatengenzwa hapa hapa nchini na kampuni ya Jerusalem Film ambayo inamilikiwa na na mimi mwenywe, hivyo sioni sababu ya wasanii kuendelea kuhangaika," alisema JB.
Alisema kuwa umefika wakati sasa wasanii wa Tanzania kusimama kwa miguu yao wenyewe bila kutegemea kubebwa na wenzao wa nje kwa vile uwezo wa kutoa filamu bora wanao na pia wana kampuni za kufanya kazi hiyo.










