Msanii huyo amesema tangu jina lake liwe kubwa kwenye muziki huo amekuwa akizushiwa mambo mbalimbali na haya ya uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya wasanii nyota ambayo alidai hayana ukweli wowote.
"Katika maisha yangu huwa sipendi sifa za kijinga kama hizo ambazo wengine wamekuwa wakizifurahia wanapoandikwa kwamba wana uhusiano wa kimapenzi na watu fulani wenye majina makubwa," amesema Baraka Da Prince.
Baraka Da Prince amesema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uhusiano wake na Nisha ambao umekuwa ikiwekwa wazi mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na Nisha mwenyewe.
"Binafsi ninatambua kwamba yapo mambo ya kuweka hadharani na pia yapo ambayo ni siri yangu mwenyewe na sina uhusiano wa kimapenzi na Nisha na hata kama ungekuwapo siwezi kuuzungumzia hadharani," amesema.
Amesema wasanii wengi wa kike ni washikaji zake tu wakiwamo Nisha, Agness Masogange, Menina na wengine wengi ambao baadhi ya watu wamekuwa wakidhani kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na vimwana hao.










