Christian Bella atimkia Ulaya

26Feb 2016
Sabato Kasika
Dar
Nipashe
Christian Bella atimkia Ulaya

MKURUGENZI wa bendi ya Malaika Music, Christian Bella amekwenda nchini Sweden kuangalia familia yake, hivyo mashabiki wake watarajie kumkosa kwa muda wa mwezi mmoja.

Christian Bella.

Mmiliki wa bendi hiyo, Daniel Denga aliiambia Nipashe jana kuwa Bella aliondoka hivi karibuni.

"Nimelazimika kutoa ufafanuzi wa safari hiyo kwa sababu kuna uvumi kwamba Bella amekimbia na bendi imesambaratika. Hakuna ukweli kwenye suala hili...Malaika Music ipo kama kawaida bila kuwapo kwa Bella," alisema Denga.

Alisema kuwa Bella ndiye anayeibeba bendi na kutokuwapo kwake jukwaani kunasababisha mashabiki kupungua.
Aliwataka mashabiki kuendelea kufika kwenye maonyesho ya Malaika Music kama kawaida.