Young Killer anayetamba na wimbo ‘Popote’ aliomshirikisha Juma Nature, amesema kuwa yeye na mpenzi wake wameshachunguzana na kudai kuwa sasa wanaweza kuishi kama mke na mume katika safari ambayo wanatarajia kuianza hivi karibuni.
Amesema kuwa hawezi kusema siku rasmi lakini muda siku yoyote ndoa inafungwa na kwamba mambo yake mengi yanabadilika kwenye maisha na kufafanua kuwa Mungu, anafungua milango kwa riziki.
Amesema anaamini kuwa hatua ya kufunga ndoa ina neema fulani na kwamba yeye na mpenzi wake huyo wanajuana vizuri na hawajakurupuka kuchukua hatua ya kuishi mum na mke.










