Katibu Mkuu wa TAFF, Methew Bicco, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa viongozi waliopo madarakani kwa sasa, wanamaliza muda wao leo.
“Utaratibu wa uchukuaji fomu ulianza Februari 3 na mwisho ilikuwa Februari 14 mwaka huu, wajumbe waliochukua fomu waliweza kujibu kiufasaha maswali yaliyokuwa yaliyokuwa kwenye kila fomu," alisema Bicco.
Bicco alitaja nafasi zitakazowaniwa kwenye uchaguzi huo kuwa ni nafasi ya urais ambayo inawaniwa na Simon Mwakifyamba na Issa Kipemba.
Nafasi nyingine ni makamu wa rais ambayo itawaniwa na mgombea pekee Deosanga Njelekela na nafasi ya ujumbe wa bodi ambayo inawaniwa na Ummy Mpallu na John Kallaghe.
Alisema wagombea hao wamepatikana baada ya kupitisha mchujo Februari 12 mwaka huu.
Bicco alisema Kamati ya Uchaguzi ilikubaliana na mgombea Abdulazizi Babu agombee nafasi ya Bodi ya Wajumbe na alikubali.
Uchaguzi huo umepangwa kuanza majira ya saa 4:00 asubuhi na matokeo kutangazwa siku hiyohiyo baada ya kura kuhesabiwa.










