Kocha huyo Mreno, aliyetwaa mataji akiwa na klabu za Porto, Chelsea na Real Madrid, hana kazi tangu Desemba mwaka jana alipotimuliwa Chelsea.
Kwa sasa, Mourinho yuko Italia kwa ajili ya kukutana na rais wa zamani wa Inter Milan, Massimo Moratti na kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba, Mreno huyo mwenye miaka 53 anaweza kurejea San Siro, lakini mwenyewe Mourinho amesisitiza kwamba hatarejea Inter kuchukua nafasi ya kocha wa sasa, Roberto Mancini.
"Timu nitakayokwenda kufundisha? Kweli sifahamu, lakini kuna uwezekanao. Napenda soka, nitarejea nikiwa na hali ileile ya kupenda soka," alisema Mourinho wakati akizungumza na La Stampa.
"Kwa sasa namheshimu kila kocha kwenye klabu. Mimi sitafuti kazi kwenye klabu, ila klabu ndiyo zinanitafuta mimi.
"Nitakapokwenda kuangalia mechi San Siro, kutakuwa na mvuto na hisia kutoka kwa mashabiki. Nataka kusema jambo moja, sitakuwa kocha ajaye wa Inter.”
Kwa muda mrefu, Mourinho amekuwa akihusishwa kwenda kuchukua nafasi ya Louis van Gaal msimu ujao.










