Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Elimu Taaluma mkoa huo, Hildegard Saganda wakati akiwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Morogoro, imeeleza kuwa hadi kufikia Februari 23 idadi ya wanafunzi walioripoti na kusajiliwa shuleni ilikuwa 46,775 sawa na asilimia 82 kati yao wavulana ni 22,203 na wasichana ni 24,572.
Ametaja halmashauri zenye wanafunzi wengi kuwa ni Kilosa ambao waliochanguliwa ni 11,156 wakati walioripoti hadi kipindi hicho walikuwa 8,990 sawa na asilimia 81 ikifuatiwa na Manispaa ya Morogoro waliochanguliwa ni 9,885 na walioripoti 7,502 sawa na asilimia 76.
Amesema, kwa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza kwa mwaka 2024 umekuwa ni wenye mafanikio makubwa .
Amesema hadi kufikia Februari 23, mwaka huu jumla ya wanafunzi wa awali 74,792 wakiwemo wavulana 37,786 na wasichana 37,006 wameandikishwa kati ya wanafunzi 93,551 ambao ni sawa na asilimia 79.95 waliotarajiwa.
Pia amesema, wanafunzi 86,408 wakiwemo wavulana 43,357 na wasichana 43,051 wameandikishwa kuanza darasa la kwanza kati ya 84,642 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 102.1
Upande wa Elimu ya awali, halmashauri ya wilaya ya Kilosa imeongoza kwa kuandikisha wanafunzi 15,588 kutoka kwenye maoteo ya idadi ya 18,063, ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya Mvomero kwa wanafunzi 10,427 kutoka kwenye maoteo ya 12,569.
Kwenye uandikishaji wa darasa la kwanza kati ya halmashauri tisa za mkoa huo , Kilosa imeweza kuongeza kuandikisha kwa wanafunzi 17, 421 tofauti na maoteo yake ya wanafunzi 16,616, ikifuatiwa na Mvomero 11,471 kutoka kwenye maoteo ya wanafunzi 11,871.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya RCC ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro,Adam Malima,aligiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu suala la elimu katika maeneo yao.










