Akizungumza na Walimu wa Shule za msingi na sekondari ambao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika halmashauri hiyo Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso amesema kuna haja ya walimu kubadilika na kufanya kazi kwa bidii bila kutegemea ajira yao.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tanganyika Hamad Mapengo amesema madeni ya walimu ni mengi hivyo wameagizwa ndani ya miaka mitatu wawe wamelipa madeni hayo ambapo amesema tayari halmashauri hiyo imetenga fedha kupitia mapato ya ndani kwaajili ya kulipa madeni ya watumishi.
Akisoma taarifa mbele ya Mgeni rasmi Mjumbe Kamati tendaji ya shirikisho la walimu ambao ni Makada wa CCM Agatha Nicholas amesema dhamira ya kuanzishwa kwa Chama hicho ni kuunganisha walimu wote chini ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuungamkono sera ya Chama hicho kwa maendeleo ya Taifa.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanganyika Yasin Kiberiti dhamira ya CCM kupitia kwa Makada wake,jumuiya zake ni kuhakikisha CCM inashinda na kuunda Dola.