Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kikosi cha Jeshi la Wananchi Kambi ya Nyumbu Kanal Charles Kalambo wakati akizungumza na wachezaji wa timu hiyo waliotambulishwa kwa wadau katika hafla ya siku ya Nyumbu iliyofanyika katika viwanja vya Nyumbu.
Kanal Kalambo pia amesisitiza nidhamu kwa wachezaji sambamba na kujitoa kwa ajili ya timu hiyo Ili iweze kufanya vizuri.
Mwenyekiti wa timu hiyo Jafar Kilindo anasema wamejipanga vizuri kuelekea mzunguko wa pili na anaamini watafanya vizuri.
Msemaji wa Nyumbu FC Mariam Songoro alisema siku hiyo ya Nyumbu iliambatana na kutambulisha jezi na kufanya harambee ambapo ahadi na fedha taslimu zaidi ya sh. Miln Tano zilipatikana.
Mariam amesema timu hiyo inakwenda kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo kutokana na maandalizi yaliyofanyika huku akiomba wadau kuendelea kuiunga mkono kwa kujitokeza kuishangilia pindi inapocheza.
Katika hafla hiyo michezo tofauti ilifanyika , ikiwa ni pamoja na kuvita kamba , kukimbiza kuku na mchezo mpira wa miguu ambapo , nyumbu veteran waliibuka kidedea dhidi ya Kibaha veterani.