Akizungumza leo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Kinana amesema Rais Samia anaonyesha njia kwa kupanga, kutafuta mikakati na kuweka vipaumbele na sasa Watanzania wanajivunia mafanikio.
Pia amebainisha kuwa wana CCM wanaposema mgombea waliyenaye anatosha kugombea mwaka 2025, hawana sababu yoyote zaidi ya kutambua mchango wake mkubwa katika taifa.
“Na Wana CCM si dhambi kusema fomu ya mgombea urais ni moja kama wanaridhika na kiongozi aliyeko madarakani. Pia CCM tuna utaratibu wetu kiongozi akichukua awamu ya kwanza anapewa kuongoza na awamu ya pili.
“Rais Samia yuko awamu ya kwanza, kwa nini asipewe awamu ya pili? Hakuna sababu ya kusema hapana. Kwa CCM kusema tumezingatia utaratibu wa chama chetu Rais anapomaliza kuongoza awamu ya kwanza anaingia ya pili,” amesema Kinana.










